Malaika, viumbe wa mbinguni wanahitaji kufanya maboresho ya haraka sana ili kuweza kuwakabili waovu wa hii dunia pale watakapokuja na bwana. Malaika wamekuwa wakitumia Mapanga kama silaha yao kuu, lakini tangia waondoke zamani hizo mwanadamu kwa kutumia werevu wake katengeneza silaha kali sana.
Silaha mpya zinazotengenezwa zinafanya silaha za malaika kupitwa na wakati. Ukilinganisha Panga na Bunduki utagundua Bunduki ni mahiri sana mwenye Panga hawezi kufua dafu.