Kenya 2022 Malala: DP Ruto anahujumu juhudi zetu za kumzolea 70% ya kura eneo la Western

Kenya 2022 Malala: DP Ruto anahujumu juhudi zetu za kumzolea 70% ya kura eneo la Western

Kenya 2022 General Election

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Malala: DP Ruto anahujumu juhudi zetu za kumzolea 70% ya kura eneo la Western

Video inayomwonyesha Cleophas Malala akimshutumu William Ruto kwa kulemaza juhudi za viongozi wa Magharibi mwa Kenya, kumzolea asilimia 70 ya kura imeibuka

Seneta huyo alidai kwamba UDA inawakandamiza viongozi wa vyama tanzu vya muungano wa Kenya Kwanza, ili wawaniaji wao waungwe mkono

Malala alidokeza kuwa ikiwa vyama vya ANC na Ford Kenya havitapewa uhuru wa kupiga kampeni mashinani, basi itakuwa vigumu kwao kumzolea Ruto asilimia 70 za kura eneo hilo

Video inayomwonyesha Seneta wa Kakamega Cleophas Malala akimshutumu Naibu Rais William Ruto kwa kulemaza juhudi za viongozi wa Magharibi mwa Kenya, kumzolea asilimia 70 ya kura kutoka eneo hilo imeibuka.

Malala alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa siasa katika kijiji cha Mwikalli, Kaunti ya Kakamega, siku ya Jumapili, Mei 15.

Seneta huyo alidai kwamba UDA inawakandamiza viongozi wa vyama tanzu vya muungano wa Kenya Kwanza, ili wawaniaji wa chama hicho cha Ruto waungwe mkono.

Malala alidokeza kuwa ikiwa vyama vya ANC na Ford Kenya vitakosa kupewa uhuru wa kupiga kampeni mashinani, basi itakuwa vigumu kwao kumzolea Ruto asilimia 70 za kura kutoka eneo hilo.

Seneta huyo ambaye anawania ugavana wa Kakamega, alishangaa ni kwa nini alikuwa akikaripiwa kwa kuwafanyia kampeni wawaniaji ANC, ilhali Kenya Kwanza iliwaidhinisha wagombea wao akiwemo seneta wa zamani Boni Khalwale.

"Hebu tuheshimiane kwa sababu baada ya uchaguzi, Ruto atasimama upande wake akiwa na watu wake sawia na Mudavadi. Hatuataki waanze kusema hawatatupea mgao wetu wa serikali kwa sababu tulishindwa kupata asilimia 70 ya kura za Western. Hatuwezi kupata asilimia 70 ikiwa hatakuwa na wabunge wetu," Seneta ahuyo aliongeza kusema.
 
Back
Top Bottom