KERO Malalamiko kwa shirika la umeme Zanzibar (ZECO)

KERO Malalamiko kwa shirika la umeme Zanzibar (ZECO)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Salaam,

Kuna kero kubwa sana kwa shirika la umeme Zanzibar (Zeco) maeneo ya shamba hasa Nungwi, Paje, Jambiani, Kendwa nk umeme ni mdogo sana baadhi ya maeneo kiasi kwamba ni kama tunaishi zama za kale, umeme mdogo mpaka unazima kuna wakati mnaweza mkalala usiku mzima hakuna umeme sio kwamba umekatika hapana umeme mdogo, wakati mwingne unazima sekunde sekunde unawaka tazama hio stabilizer hapo umeme unasoma voltage 114 ikishuka zaidi ya Voltage 100 mita inazima.

Mita walizoweka haswa mpya umeme ukiwa chini ya volts 100 zinajizima kinachokuja kutokea mnakaa kiza
Ni kheri feni, friji nk zisifanye kazi lakini taa ziwe zinawaka lakin hio haipo baadhi ya maeneo hayo umeme unazima kwa kawaida tumezoea kukaa giza.

Namba walizoweka huduma kwa wateja haijwahi kupokelewa hata siku moja na namba waliyoweka kwa ajili ya wilaya ya kusini na kaskazini haijawahi kupatikana hatuna hata pa kupelela kero tukienda ofisini walau watubadilishie mita kama za zaman ambazo umeme hauzimi wanasema hizo mita hazipo.

Hii kero kubwa sana , tunakaa giza kila siku hatuna umeme wanaopata walau umeme ni wale walio karibu na transforma au wenye pesa walionunua transforma binafsi sisi ambao hatupo hapo ni kukaa giza kila siku.

Tunaimba tupaze sauti , umeme kuwa mdogo zanzibar ni sawa tatizo la kote lakini sisi kero kubwa kwanini tunakaa giza bora hata taa tu ziwe zinawaka.

Angalau wenzetu wa mjini umeme hauzimi na kuwaka kama huku shamba , licha ya kuwa na stabilizer lakin haisaidii kitu.

Wanaopitia hii changamoto wanaelewa imagine kila siku usiku tunawaza mshumaa kama zama za kale na hili tatizo sio la wiki au mwezi tumezoea huu mwaka sasa.

Msaada kupaza sauti walau watuongezee ata transforma na sisi tupate hata mwanga tu kama wenzetu tunateseka sana sio kidogo na hakuna pa kupaza sauti zetu

IMG_2779.jpeg
 
Back
Top Bottom