SoC02 Malalamiko na Mafadhaiko hayatabadili Maisha yetu: Somo kutoka kwenye TOZO na Kupanda kwa gharama za Maisha

SoC02 Malalamiko na Mafadhaiko hayatabadili Maisha yetu: Somo kutoka kwenye TOZO na Kupanda kwa gharama za Maisha

Stories of Change - 2022 Competition

Spellbinder

Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
7
Reaction score
12
Habari yako mpambanaji mwenzangu?. Karibu katika makala hii inayohusu kupigana vita ya kuyasaka mafanikio.

Labda kwa ufupi ningependa kukumbusha kuhusu Maisha. Wakati kila mtu ana namna yake ya Kuyaelezea maisha, kwangu mimi, Maisha ni kama vita. Usipojiandaa vema kupigana, maisha yatakupiga hadi uishe kama kipande cha kuni kigeukavyo kuwa majivu kwenye moto mkali.

Nimeandaa mtiririko mzuri wa namna ya kuzishinda changamoto na hali ngumu ya Maisha kadri tujongeavyo katika kukifikia kilele cha Mafanikio.

Kwa kuanza, tuangazie suala la Fikra, Mitazamo na Mawazo. Nadhani hutapingana na mimi kuwa Fikra ndio kila kitu linapokuja suala zima la Mafanikio. Haijalishi umejaaliwa vipaji vingapi au unazungukwa na kina nani, kama utakosa fikra yakinifu si rahisi kudumu na kitu chochote. Kwa hiyo kabla ya yote ni vema kuchagua fikra za ushindi kuliko fikra za ukosaji. Tuwe na imani ya ushindi.

Pili, ni vema kujiwekea malengo sahihi. Kwa mfano lazima ujitambue we ni nani?, umetoka wapi? unaenda wapi? na unatakiwa ufanye ni nini ili kufika hapo unapotarajia kufika?. Naomba nikukumbushe kuwa bila kujitambua na kuwa na nidhamu juu ya Malengo yako uliyojiwekea, sio rahisi kuyafikia mafanikio.

Sasa nirudi kwenye mada kuu, ambayo ni hali halisi tunayopitia kwa sasa.

Kutokana na Mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO-19 pamoja na Vita kati ya Urusi na Ukraine, tumeshuhudia kupanda kwa gharama za maisha na kuongezeka kwa TOZO na kodi. Ukiwa dhaifu utaishia kulaumu tu, na kama ilivo desturi kulaumu tu hakubadilishi chochote, zaidi ya kuongeza sonona na mafadhaiko moyoni, hali ambayo inaweza kuongeza msongo wa mawazo na pengine kujitoa uhai.

Lakini, kabla hatujaendelea naomba nikukumbushe kuwa; wakati huu ambapo uchumi umeyumba kuna wanaofanikiwa kupitia hizi changamoto, wakati huohuo pia kuna wanaoshindwa kuendelea.

Hivyo, nadhani huu ndo wakati wa kupambana na kuvishinda vikwazo. Wakati wengine wakilalamika na kuilaumu serikali, wewe kuwa wa kipekee. Tumia muda huu kukaa na kuzichungulia fursa. Tumia huu muda kujifunza ujuzi utakaokusaidia kutatua changamoto za watu.

Najua kuna mtu anafikiria kwamba labda mimi naunga mkono suala la kuanzishwa Kwa tozo mpya na kupanda kwa gharama za maisha. La hasha! Mantiki yangu hapa no kwamba tusipoteze muda na nguvu nyingi kwenye kulaumu. Bali tuendelee kupambana licha ya magumu tinayoyapitia kwani kulaumu tu hakutasaidia kubadili Maisha yetu.

Hakuna siku ambayo utakuja kusema gharama za maisha Zimekuwa kama unavotaka. Yani kwamba kila mmoja wetu aridhike na kufurahi kuwa anaishi maisha na kutimiza mahitaji yake kikamilifu.

Unakumbuka Mwana FA katika wimbo wake wa 'GWIJI' aliwahi kusema "Dunia haitasimama ukigoma Kutembea nayo" Vivyo hivyo watu hawataacha kufanya Biashara Kwa sababu ya kuongezeka kwa Tozo. Watu hawataacha kununua vocha eti kisa vifurushi vimepanda bei, watu hawataacha kuendesha magari eti kisa Mafuta yamepanda bei. Nadhani utaungana na mimi kuwa ukienda kwenye maeneo ya starehe utakuta watu wakunywa pombe na kupiga misosi kama kawaida.

Wakati wewe unaona vikwazo vya kutimiza ndoto zako, mwingine anaitumia kama fursa ya kutimiza ndoto zake. Maisha huja kama tunavyoyatengeneza. Hivyo tufanye kazi kwa bidii na tuweke akiba katika kidogo tunachopata.

Hakuna cha bure, chochote unachotaka lazima ukifanyie kazi. Kama unataka kitu fulani ni lazima ufanye kazi kwa bidii. Kazi yako ndo malipo yako.

Chaguo unalofanya katika maisha litafanya umaskini uishe au uendelee.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom