Malalamiko: TIGO Mmeamua Kutuibia Wateja Wenu? Tutashitaki TCRA

Malalamiko: TIGO Mmeamua Kutuibia Wateja Wenu? Tutashitaki TCRA

Albedo

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Posts
5,558
Reaction score
1,456
TIGO sasa naona wamelewa sifa na sasa wanatufanya wateja wao kuwa ni Mazuzu tusiojua Taratibu na Sheria za Nchi, "TUTAWASHITAKI". Siku hizi ukimpigia Mtu wa Tigo kama Hapatikani wanakwambia Bonyeza 0 kuacha Ujumbe wa Maneno lakini hata kama Usipobonyeza 0 kukubali jamaa wanakupeleka moja kwa moja kwenye Voice Message na UNAKATWA PESA! Tigo Mmetuchuka wateja wenu kiasi hiki? Hakya Mungu Mkiendelea hivyo nawageuza "DILI" Nitawashitaki TCRA na ninauhakika Nitakula Hela Nzuri tu ya FIDIA

Nawapa Siku Saba Mrekebishe hiyo hali kwamba kama Mtu hajachagua namba ya kukubali kuacha Ujumbe wa Maneno Msimlazimishe, Msiporekebisha tutakuna CCC

Habari ndiyo hiyo
 
Thameni tusizozane nao mimi siku hizi toka waanze utaratibu wao nahamasisha watu kuachana nao. Na kila nayemkuta anatumia tigo namweleza kuwa hawa jamaa ni wezi inawezekana kuwaua kibiashara kwanza hawako reliable hawa. Na network yao ipo Dar tu, ngoja mimi kwa sasa najaribu airtel na voda
 
Duh Airtel mnapeta sana kwasasa. Tunahamia airtel sasa. yaani mpaka tigo muje mushtuke Airtel atakua ameliteka soko jumla jumla. I wish airtel mnge grab hii opportunity faster
 
Duh Airtel mnapeta sana kwasasa. Tunahamia airtel sasa. yaani mpaka tigo muje mushtuke Airtel atakua ameliteka soko jumla jumla. I wish airtel mnge grab hii opportunity faster

Yaani niko sooo Desperate na huu Mtandao! Very Soon NITAHAMIA ila ni baada ya kula hela ya hawa Wajinga
 
Duh Airtel mnapeta sana kwasasa. Tunahamia airtel sasa. yaani mpaka tigo muje mushtuke Airtel atakua ameliteka soko jumla jumla. I wish airtel mnge grab hii opportunity faster

Seconded
 
Hawa jamaa sasa siwakubali line yao nimeiweka kwenye kabati la magazeti ninayotegemea kuyachoma
 
Kama kweli wao waungwana ujumbe wameupata kwani haya ndio mawazo yetu watanzania.kusema kweli wanaboa
 
Kama kuna mtandao una maudhi hapa bongo, huu nadhani unaongoza, jamaa wamekaa kisanii sana yani mpaka unakera, yani line yao nshaiweka kapuni long.
 
zaidi ya kutuibia kupitia voice message pia wanaiba kwenye gharama kwa sekunde, badala ya sh 1 kwa sekunde sasa wanachaji zaidi japo wanaendelea kutangaza sh 1 kwa sekunde, niliweka sh 2000 nikaongea na mtu kwa dk 12 pesa ikaisha kabisa kitu ambacho si sawa, ilipaswa kuwa chini ya sh 1000..!
 
jamani inaweza kuwa mtumiaji ndio kakuweka kwa blacklist, msiwalaumu tigo watu ambao huwa hawapendi kusumbuliwa huweka voice mail
 
Back
Top Bottom