Strange, wakati wengine wakibishana ubora wa Vyuo vyao, kuna watu wako bize ile mbaya kikisiriba Chuo hicho!
Kwa maoni yangu, baada ya kupitia nyuzi kadhaa za kusiriba hicho Chuo, Wasiribaji wanaongozwa zaidi na chuki binafsi kiasi cha kuwafanya wasistahili kuitwa whistleblowers.
Hali hii ina athari nyingi sana kwa Chuo au Taasisi. Mojawapo, baadhi ya Maofisa Uajiri wanaingia JF. Picha wanayoipata kwa Chuo kutoka na maandishi juu ya Chuo inaweza kuathiri fikra zao juu ya Wahitimu wa Chuo hicho. Nina uzoefu na hilo - miaka kadhaa iliyopita nikiwa katika jopo la ajira ktk NGO moja ya KiMarekani, tuliwaengua Waombaji Kazi, waliokuwa wameshinda hatua kadhaa za Usaili, kwa sababu za sifa mbaya tuliziona katika mtandao kihusishwa na Chuo kama Taasisi.
Kwa Wazazi, Walezi, n.k., watakuwa na haki ya kusita kuruhusu Watoto kujiunga na Chuo hicho kwa sababu Chuo kimepakwa karibu kila aina ya uchafu hasa kupitia JF!
Something must be done, and, immediately!