Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Malamba Mawili Msikitini hakuna maji bombani kwa miezi miwili, DAWASA ukiwapigia wanajibu wamepokea taarifa wataiwasilisha sehemu husika inaishia hapo, ukipiga tena wanakuuliza taarifa mpya kabisa na wanasema ndio taarifa ya kupokea, ni kama ukimaliza kuongea nao hakuna chochote wanachofanya.
Kila muhudumu anaonesha kutokuwa na taarifa, ina maana huwa wanajibu tu kuonesha wamejibu baada ya hapo wanaendelea na maisha yao hawajali wala hawachukui hatua ndio maana kila mtu anajibu mara tutatuma mafundi, mara tutatuma wataalamu waje kujua tatizo, mara tunapeleka taarifa sehemu husika ifanyiwe kazi na kila mtu na jibu lake na inabidi ueleze shida upya huku akionesha kutokuwepo kwa taarifa za jambo hilo na unakuwa usharipoti zaidi ya mara moja.
Huku maji hayatoki bombani miezi miwili sasa ila wanatuma bili na kutaka zilipwe, na maji hawaleti, kifupi hawatambui kuwa maji ni huduma ya muhimu sana ambayo haikutakiwa kuletewa mzaha. Kwa nini hamleti maji? Yaani mnakaa mwezi hamjasukuma maji mnategemea watu waishije? Au kuna mbadala wa maji tuambieni basi maana mngejua hakuna mbadala msingetulia tu na hamjaleta maji miezi miwili licha ya wananchi kuwapa taarifa ya kukosa huduma.
Tanzania leo bado tunahangaika na kitu kinaitwa maji tena Dar, Aibu sana na uchungu mwingi kwetu wananchi sijui kwa nini mnatuchukulia kama hatuna umuhimu wa kupewa huduma za muhimu, tunajikuta tunaingia gharama kubwa za kununua maji Lita 1000 kwa 20000 mpaka 25000, au ununue ya kwenye madimbwi kwa lita 1000 ambayo sawa na 15000, hivi mnataka tufe kwa magonjwa kwa kutumia maji machafu?
Wizara ya Maji na DAWASA Mna mpango gani na Malamba Mawili msikitini? Au mnataka tufe kwa magonjwa ya mlipuko kwa kutumia maji machafu? Au mnafurahia tunavyonunua maji kwenye yale magari ambayo madumu hata kuoshwa sijui kama yanaoshwa? Au mnaona raha tunavyohangaika na ndoo vichwani?
Kama mnaona hamuwezi kutuletea maji semeni mmeshindwa ili tufute mawazo kuwa tuna mabomba basi maana hayana faida.
Pia soma:DOKEZO - Maji Malamba Mawili hayajatoka kwa mwezi 1 sasa, shida nini?