Wakazi wanaamini Vyandarua vya Serikali vinaleta Kunguni na kupunguza nguvu za Kiume
Wakazi wengi wa mkoa huu ni fukara ambapo kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), wakishika nafasi ya pili kwa ‘umasikini’ mkubwa kwa kaya nchini. Umasikini huo unachochea imani ambazo zinakinzana na sayansi, hivyo kuongeza madhila ya maisha kwa familia nyingi.
Mathalan, baadhi ya Wananchi wa mkoa huu hawatumii vyandarua vyenye dawa. Hii ni kutokana na kusambaa kwa imani potofu kuwa dawa iliyomo, inaweza kuwa na athari kiafya. Jambo hilo, linaufanya mkoa huu kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria nchini.
Kwa mujibu wa tovuti ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, idadi ya wagonjwa wanaokutwa na maambukizi ya malaria imeongezeka kila mwaka kipindi cha mwaka 2019-2022. Hali inayoifanya Wilaya hiyo kuwa kinara nchini kwa maambukizi ya malaria. Kabla ya matokeo mapya ya utafiti uliowasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, mwaka 2023 kuonesha kuwa kinara kwa sasa ni Kibondo, Wilaya nyingine ya Kigoma.
Uchunguzi umebainisha kuwa, wananchi wa wilaya za Kakonko, Kibondo na Kasulu, zenye kiwango kikubwa cha malaria, wamekuwa wakikwepa kutumia vyandarua vyenye dawa kwa madai kuwa, vinapunguza nguvu za kiume. Wengine wakiamini kuwa vinasababisa wanawake kushindwa kushika mimba pamoja na kusababisha kuwepo kwa ongezeko la wadudu kama kunguni, majumbani mwao.
Madai hayo ya jamii yamesababisha vyandarua vinavyosambazwa na serikali, kuachwa majumbani bila matumizi, huku wengine wakivitumia kama uzio kwenye bafu au choo, pamoja na kukinga bustani za mboga, ili kuzuia mifugo hususan kuku na bata. Wengine wamevihifadhi ndani, bila matumizi.
Jen Samandari (28) (jina siyo halisi) mkazi wa Kakonko mjini anasisitiza kuwa hawezi kutumia vyandarua hivyo. Anaamini kuwa, dawa iliyowekwa kwenye vyandarau kwa ajili ya kuua mbu, inaleta kunguni majumbani mwao. Anasema, “Mimi kamwe siwezi kutumia hivyo vyandarua vya serikali, kwanza havina muonekano mzuri, vina harufu mbaya na ni chanzo cha kunguni, na wanaotumia wanakiri vinawahi kuharibika kwa kujikunjakunja na kutengeneza maficho ya kunguni.”
…Sijui wanaweka madawa gani kwenye hizo net zao, siwezi, mimi bora nilale bila chandarua,” ni kauli na mama mwingine mkazi wa Kakonko ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, huku akionesha chumba kimojawapo ambacho kina kunguni.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kakonko, Frida Anderson anabainisha kuwa ofisi yake imekuwa ikipokea taarifa kutoka kwa wahudumu wa afya ya jamii kuhusu upinzani wa matumizi ya vyandarua kutokana na dhana potofu.
“Tangu tuanze mkakati wa kugawa vyandarua vyenye dawa, pamoja na kupulizia dawa ya kuuwa wadudu majumbani, tulishuhudia kiwango cha malaria kikipungua, lakini baada ya muda, ugonjwa huo ukapamba moto......Tunakabiliana na upinzani mkubwa wa imani potofu, ambapo jamii inaamini kwamba, ukilala ndani ya chandarua, unaota ndoto mbaya...Wengine wanahisi kuwa, dawa zilizowekwa ndani ya chandarua, zina madhara ambayo eti yanaweza kusababisha watoto wao washindwe kupata uzazi,” anaongeza Frida.
Naye Rosa Samsoni (57), mhudumu wa afya ya jamii Kakonko, amesema elimu imekuwa ikitolewa na kuwafikia wananchi, hata hivyo, imani potofu husambaa zaidi kuliko uhalisia.
Anasema “Tunapotoa elimu nyumba kwa nyumba kuhusu masuala mbalimbali ya afya ya jamii, tunakutana na hoja nyingi kinzani. Mfano, Wanaume wengi hudai kwamba vyandarua hivyo, vinasababisha kupungua kwa nguvu za kiume, huku wengine wakieleza kuwa wakilala ndani ya chandarua, hukosa usingizi au kuona maluweluwe nyakati za usiku,”
Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Jesca Leba anakaili kuwepo kwa uvumi hasi kuhusu vyandarua na madawa ya ukoko na kueleza kuwa Imani potofu na ushirikina miongoi mwa wananchi wa Kigoma ni miongoni mwa sababu za mkoa huo kuendelea kuwa katika orodha ya juu ya mikoa yenye maambukizi mengi ya malaria nchini

Upvote
0