Hivi malaria inaweza kusababisha kuona mauza uza na kuota ndoto za ajabu?
Yaani ndoto za kutisha na kuwa na wasiwasi uliopitiliza
Pia mauza uza hasa ya kukabwa shingo, chumba kuwaka moto n.k
Nawasilisha
Yaani ndoto za kutisha na kuwa na wasiwasi uliopitiliza
Pia mauza uza hasa ya kukabwa shingo, chumba kuwaka moto n.k
Nawasilisha
- Tunachokijua
- Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya Plasmodium ambavyo husambazwa na mbu.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mwaka 2021 pekee, zaidi ya visa vya Malaria milioni 247 viliripotiwa kutokea duniani, ambapo watu 619,000 walipoteza uhai kutokana na maambukizi hayo.
Ingawa maelezo ya mapema ya athari za kiakili za malaria yalionekana kwa mara ya kwanza katika fasihi ya kale ya matibabu ya Hippocrates na Galen, ilichukua karne nyingi baadae ambapo maelezo ya athari hizi yalifahamika zaidi.
Taarifa za kina zilienea sana baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia (WWI), ambapo Malaria, janga la eneo la Makedonia, kati ya mwaka 1916 na 1918, ilionekana bila kutarajiwa kuwa sababu kuu ya magonjwa ya akili miongoni mwa askari waliopigana maeneo hayo.
Tangu miaka hiyo, tafiti nyingi za afya zimeelezea baadhi ya athari kama kusahau na kuchanganyikiwa kwa watu wanaopatwa na Malaria kali. Pia, maambukizi ya malaria ya muda mrefu au ya muda mfupi yametajwa kuwa na uwezo wa kusababisha mfadhaiko, wenge, wasiwasi, vurugu, fadhaa, kukosa usingizi na kuota ndoto mbaya.
Hivyo, kwa kuzingatia rejea hizi, pamoja na maelezo mengine ya kitaalamu ambayo JamiiForums imepata, imebainika kuwa ugonjwa wa Malaria unaweza kumsababishia mhusika aone mauzauza na kuota ndoto mbaya (za ajabu).