Malaria sugu inanitesa! Dawa gani itanipa tiba ya kudumu?

There is a saying," an apple a day keeps a doctor away." the best solution is to make your young sister improve her own immune system. Medicines are just helping the immune system to fight infections, and doctors of tommorow wil not use drugs to treat patients bt wil use fruits and vegetables to treat their patients, pm me for free consultation or call 0752720276 to know how you can build a strong body immunity and reduce succeptibility to infections and improve your cardiovascular functions.
 
Dah!Mkuu REX,kwanini usimwage maujuzi hapa jamvini tufaidi sote?
 
Last edited by a moderator:
Wandugu mdogo wangu amekuwa na tatizo yani haipiti wiki 3 lazima aumwe malaria tumeshabadilisha dawa za kila namna lakini wapi mwenye uwezo wa kutusaidia tatizo atuambie jamani

hiyo ni malaria sugu ambayo kupona kwake kuna hitaji tiba mbadala sikia nakupa dawa ya kiswahili,,,,,chukua magome ya mti wa muembe,,,,,,chukua majani ya mpela mwekundu au hata mweupe ukikosa mwekundu nnaposema mpela mwekundu namansha ukipasua pela lake utakuta ndan jekundu,,,,,, ukishachukua hayo magome na majan ya mpela bac yaoshe kawa maji safi kisha yatie katka sufuria yachemsha mpaka yachemke haswa kisha chukua maji yake ambayo yatakuwa na rangi kama ya udongo au damu ya mzee au brown colour yatie katka chupa au chomba utakachoona kinafaa na anywe kikombe kimoja kutwa mara tau au hata mbili nna iman itaondoka hiyo malaria,,,,,,,,
 
Ninayo dawa ya asili ya malaria sugu, ukinywa unaweza kukaa hata miaka 6 bila kuuguwa malaria, ninauhakika nayo 100% na ikitokea umekunywa na ukaugua tena malaria ndani ya miezi 6 nitakurudishia pesa yako. Nipigie 0714755582, nipo dar.
 
naona wewe tatizo lako linatokana na mlo wako.dawa ni sumu zikikzidi, hivyo huna haja ya kuendelea kula dawa za malaria. jaribu kuboresha mlo wako uwe balance na upunguze stress zinazoupata mwili kama kazi ngumu sana, pombe kali, kutokulala mapema, kukaa na njaa muda mrefu. pia usisahau maombi.
 
Kuna mtu aliniambia maji ya dafu ukichanganya na ndimu ni dawa ya malaria ila sina uhakika labda MziziMkavu aje atueleze kama hyo tiba ni kweli
 
Last edited by a moderator:
Kuna mtu aliniambia maji ya dafu ukichanganya na ndimu ni dawa ya malaria ila sina uhakika labda MziziMkavu aje atueleze kama hyo tiba ni kweli
Mkuu King Kong III nijuavyo mimi ndimu ina idadi zake ukipata na kuitengeneza inatibu malaria sijajuwa kuwa maji yamdamu uchanganye na Dafu kuwa inatibu malaria hiyo ninakusikia wewe leo. Zipo dawa nyingi tu za kienyeji za kutibu ugonjwa wa Malaria mojawapo ni Mjani ya Mti wa muarubaini unatibu ugonjwa wa malaria na ingine dawa nyingi tu za kienyeji zinaweza kutibu ugonjwa wa Malaria.
 
Nilikuwa na tatizo kama lako karibu miaka 10 iliyopita nikatumia asali na mdalasini kila asubuhi na jioni. Kijiko kidogo kimoja cha asali changanya na robo kijiko mdalasini au utakavyoona mchanganyiko mzuri kwako. Tumia mwezi mmoja au zaidi. Asali ina sifa ya kuogeza kinga mwilini yaani uwezo wa mwili kujilinda maradhi. hata hivyo endelea kutumia dawa za maralia kama kawaida. Mungu asakusaidia. Nina miaka karibu kumi sasa maralia hainisumbui tena. Kabla ya hapo nilitumia dawa mbalimbali za maralia kama fasida, halfan, zandu nakadhalika bila mafanikio.
 
Wakuu si mara ya kwanza kuja hapa kuomba ushauri wenu!!

Kwa kifupi ni kama miaka miwili na ushee sasa sijawahi kuwa mzima kutokana na huu ugonjwa!! Nimefanya vipimo vyote ila huwa nakutwa na malaria peke yake na mara chache minyoo. Nimetumia dawa nyingi kuanzia za hospitalin mpaka miti shamba, ila hata pale nilipoweza kutokomeza wadudu wote...sikuweza kurudi kwenye normal condition na malaria ilirudi tena ndani ya mwezi ama miezi miwili.

Ninavyoandika hii thread, ndani ya mwezi nimetumia dawa zaid ya 3 hakuna mafanikio yeyote. Nilianza na Malafin ikachemka, nikanywa Atequin nayo haikunipa nafuu, nikaandikiwa vidonge vya quinin bado sikuona unafuu, hivi wiki iliyopita nimepima na kuktwa na malaria 5, nimekunywa Duo-cotexin lakin mpaka muda huu hali haijatengamaa!!

Najitahidi kwa kila hali kuwakwepa mbu lakini haisaidii, wengine wanasema ni malaria sugu...sikatai inawezekana...ninachowaomba, mwenye uwezo wa kunifanya nipate tiba sahihi anisaidie...niondokane na haya masumbuko..

Sina raha ndugu zangu, hata kazi nafanya kwa kujilazimisha!!

Asanteni!!!
 


KWA UFUPI

  • Hofu itakuja pale wananchi watakapoanza kujiuliza kuhusu madhara wanayoweza kuwa wameyapata kutokana na matumizi ya dawa hiyo.


Zipo taarifa kwamba Serikali iko mbioni kubadilisha sera na miongozo yake kuhusu tiba na uchunguzi wa ugonjwa wa malaria ili dawa mpya ya Artesunate ianze kutumika kutibu malaria kali badala ya Quinine. Kwa vyovyote vile, taarifa hizo zitaleta mkanganyiko na hofu miongoni mwa wananchi, kwani hatua hiyo ya Serikali inaweza kutafsiriwa kwamba dawa ya Quinine imeshindwa kutibu ugonjwa huo sugu na kwamba imekuwa ikitumiwa tu kama majaribio.

Wasiwasi na hofu inayoweza kuwagubika wananchi kutokana na hatua hiyo ya Serikali inaeleweka. Kwanza, ugonjwa huo ndiyo unaoua watu wengi zaidi katika nchi maskini kama Tanzania kuliko ugonjwa mwingine wowote.

Hapa nyumbani, takwimu zinaonyesha kwamba watu wapatao 80,000 hufariki dunia kila mwaka na wengine milioni 12 huugua ugonjwa huo katika kipindi hicho. Kwa mujibu wa takwimu, asilimia 40 ya wagonjwa ambao huripoti katika vituo vya afya kila mwaka hufanya hivyo kwa kusumbuliwa na malaria.

Jambo la pili ni kwamba kubadilishwa kwa dawa hiyo ya Quinine na badala yake kutumia Artesunate kunaweza kutafsiriwa na wananchi wengi wa kawaida kwamba Quinine ambayo imekuwa ikitumika kwa miongo mingi imeshindwa kutibu ugonjwa huo. Hofu itakuja pale wananchi watakapoanza kujiuliza kuhusu madhara wanayoweza kuwa wameyapata kutokana na matumizi ya dawa hiyo.

Hapo ndipo zitakapoibuka hisia kwamba miili yao imekuwa ikitumika muda wote huo kufanya majaribio ya dawa hiyo ya Quinine.

Ni jinsi gani basi wananchi watapokea ujio wa dawa hiyo ya Artesunate katika mazingira kama hayo ni swali linalosubiri wakati. Huko nyuma wananchi walishuhudia Serikali ikiziondoa sokoni dawa kadhaa za kutibu malaria moja baada ya nyingine, ikiwa ni pamoja na Chloroquine, Fansida na Dawa Mseto (Alu), kwa maelezo kwamba vimelea vya ugonjwa huo vimekuwa sugu kwa dawa hizo. Unahitajika utafiti wa kutosha kabla dawa hazijapitishwa kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Hoja tunayotaka kujenga hapa ni kwamba Serikali imefanya makosa makubwa kuelekeza nguvu na rasilimali nyingi katika kutafuta tiba ya malaria badala ya kutafuta chanzo chake kwa kutokomeza mazalio ya mbu. Tumekuwa tukijidanganya kwa kudhani kwamba tutatokomeza ugonjwa huo kwa kusambaza vyandarua au kubadilisha dawa za kutibu malaria. Inaonekana tunafanya hivyo makusudi au hatujui kwamba gharama za kuzuia malaria ni ndogo mno kuliko gharama za kuitibu.

Katika miaka ya 80 Serikali ya Japan ilibuni na kufadhili mradi wa kunyunyizia dawa katika mazalio ya mbu hapa nchini. Hata hivyo, mradi huo ulihujumiwa kwa sababu uligusa masilahi ya wakubwa waliokuwa wakineemeka na uingizaji nchini wa dawa za kutibu malaria. Ndiyo maana ugonjwa wa malaria unaendelea kudunda na kusababisha maafa tuliyoyataja hapo juu.

Tunaambiwa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), limepanga kujenga kiwanda mkoani Pwani cha kutengeneza dawa za kuangamiza mazalio ya mbu. Jambo la ajabu ni kwamba mpango huo unapigwa vita kila kona kwa sababu unagusa masilahi ya kundi fulani. Badala yake, tunaambiwa Serikali inahaha huku na kule kuhakikisha sera na miongozo yake kuhusu tiba ya Malaria zinabadilishwa haraka ili dawa mpya ya Artesunate ianze kutumiwa mwezi huu badala ya Quinine. Bila shaka wanaofaidika na mradi huo watakuwa wakisema kimya kimya: ‘Udumu ugonjwa wa malaria’.
Chanzo. Tiba ya Malaria bado inatupiga chenga - Uchambuzi - mwananchi.co.tz




 
Badala ya kuhangaika kutafuta dawa tu tuweke juhudi katika kupambana na ongezeko la Mbu nchini kwa kuhakikisha maeneo yote ya maji ya mvua yaliyosimama yanatiwa dawa ambazo zitaondoa uwezekano wa mbu kuzaliana, mifereji kusafishwa ili kuhakikisha maji ya mvua hayapati nafasi ya kusimama na kuwa vyanzo vya sehemu ambazo mbu wanaweza kuzaliana, vichaka karibu na maeneo wanayoishi watu vinasafishwa ili kuondoa maeneo ambayo mbu wanaweza kujificha tayari kufanya mashambulizi yao. Siku zote kinga ni rahisi mno kuliko tiba.
 
MIMI NINACHOSHAURI NI KUTUMIA TEKNOLOJIA ILE ILIYOTUMIA KWA MBUNG'O PALE KANGE MKOANI TANGA KUZAZISHA

MADUME MENGI YA MBU AMBAYO NI TASA HAYA YATASHINDWA KURUTUBISHA MAYAI YA MBU JIKE KWA MSINGI HUO MAYAI

YOTE YATAKAYOTAGWA YATAKUWA VIZA WALA HAKUNA KUHARIBU MAZALIA YAO KUFYEKA AU KUHARIBU MAZINGIRA SHIDA

WASOME WAZURI BADALA YA KUBAKI KWENYE TAASISI ZA ELIMU WAFANYE UTAFITI WANAKIMBILIA BUNGENI KUBWABWAJA

SHIDA YA MAENDELEO DUNI TANZANIA NI UVIVU WA KUFIKIRI NDIO SABABU RASILIMALI WATU NI SAWA NA SIFURI.MKUU.@
BAK
 


Uyasemao ni kweli kwani sie watanzania tumehalalisha uchafu kuwa fenicha maana usipo ona uchafu basi siku yako haiendi vizuri.
 
MziziMkavu unakumbuka mwaka juzi mlifuga mbu hapo jangwani kwa lengo kama hili ulilolisema hapa chini,
nashangaa ule utafiti ulishindikana na wakafungulia wale mbu wakazaa kila mahali hadi muhimbili wagonjwa walihangaika sana, sie wakazi wa jangwani ndo loo,

tz sijui kwanini wataalam wetu wanakuwa hivyo, wakishapokea 10% zao wanaishia chama sema lolote kuhusu hili hapa.

Sijui ulikuwa mradi wa nchi gani, au ndo miradi ya clinton sijui.

 
Last edited by a moderator:
Kibongo bongo ukipata malaria ole wako uanze hiyo dozi ya kujitibu
unaugua unakaribia kufa, mmmmh, hii nchi ni noma kila upande.
 
Mamndenyi
vita dhidi ya mbu ni rahisi sana nakumbuka zama hizo watu walikuwa wakishiriki kwa pamoja kusafisha mazingira; kufukia madimbwi; kusafisha mifereji; siku hizi mjumbe wa mtaa akiwa CCM Chadema watagoma kushiriki; jamani hata huku tunasafisha mazingira yetu community service tunajitolea angalau mara moja kwa mwezi; familia zote zinashiriki hakuna anayeuliza mbona kodi tumekatwa huo ndio uzalendo!
 
Last edited by a moderator:
......na siku dawa ikipatikana lazima ikafanyiwe uchunguzi huko kwao
 
chama umenikumbusha;
kweli tena wakati mwingine tulikuwa tunaitwa na ile pembe tunaenda kufanya kazi za kujitegemea,

Huko kwetu vijijini hii bado ipo, tuna siku ya kufanya usafi; pia tuna miti kama mlonge ambao ukiwa unakula majani yake wala nusu kiganja mara moja kwa wiki hautakaa ukaugua malaria, tatizo ni huko mjini kwenu.

Nikwambie kuna mtaa mmoja huko kwenu dar waliamua kuchonga barabara za mtaa,
kwa kuwa mbunge ni chadema; eneo analoishi diwani wa ccm lilipitwa bila kukwanguliwa,
kweli vituko haviichi bongo.

 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…