Malaria yawasumbua watafiti

Malaria yawasumbua watafiti

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa (NIMR) kwa kushirikiana na watafiti wengine wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, inahangaika kupata majibu ya kwa nini maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini yameshuka kutoka asilimia 80 kwa miaka ya nyuma hadi kufikia chini ya asilimia 10.<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->Kaimu Mkurugenzi wa NIMR, Dk Julius Masaga alitoa taarifa hiyo jana kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii walipotaka kujua ni sababu zipi za kitaalamu zilizosababisha kushuka kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->Wajumbe hao wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wao, Kebwe Stephen Kebwe ambaye ni mbunge wa jimbo la Sengerema wapo mkoani hapa kutembelea vituo vinavyoendeshwa na taasisi hiyo ya NIMR.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->Aliyeuliza swali hilo ni Mbunge wa Viti Maalumu Singida, Martha Mlata aliyetaka kujua kama utafiti umefanyika kitaalamu kujua kwa nini malaria yamepungua kwa kiasi kikubwa namna hiyo.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->“Hadi sasa hakuna majibu ya moja kwa moja ya kwa nini maambukizi ya malaria yamepungua kwa asilimia hizo, hata sisi imetushangaza na ndiyo maana kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Wizara ya Afya na taasisi nyingine tunahaha kufanya utafiti,” alisema Dk Masaga.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->Alisema wengi wanadhani ni kwa sababu ya matumizi ya vyandarua, lakini inaweza kuwa ni sehemu tu, lakini sisi kwenye utafiti inabidi tumuangalie pia mbu tujue na mambo mengine mengi ya kitaalamu ili kuweza kupata majibu.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->Kaimu Mkurugenzi huyo aliwaambia wabunge hao kuwa kitaalamu kuporomoka kwa maambukizi ya malaria ni changamoto kwani inaweza kuwa ni tatizo kubwa kuliko ilivyokuwa awali ambapo walijikita katika kuwatibu wanaougua.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->Wakiwa katika maabara ya NIMR Tanga,wabunge hao walielezwa na Mkuu wa Mabara na kitengo cha utafiti wa magonjwa wa kituo hicho, Dk Jeros

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->Ishengoma kuwa wakati malaria imeshuka hadi kufikia asilimia ya chini ya 10 lakini bado kuna ongezeko la homa.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->“Hili swali bado halijajibiwa na jukumu hili linatukabili watafiti

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->kujua sababu na kupata majibu,hadi sasa hatujajua ni nini kimeondoa malaria huku homa likiwa bado tatizo”alisema Dk Ishengoma.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->Wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya NIMR,wabunge wa kamati hiyo



walishauri Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuweka utaratibu wa kuwafundisha vijana wapate ujuzi wa kukarabati vifaa ambavyo vinaharibika katika maabara mbalimbali nchini.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->Walisema tatizo la kuharibika kwa vifaa vya maabara ni kubwa kwani vinapoharibika husubiri hadi wataalamu kutoka Ulaya au Afrika kusini waje kuvitengeneza wakati kungekuwa na utararibu wa

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->kuwafundisha vijana waliopo nchini ingepunguza gharama na kutoa ajira kwa Watanzania.

<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->



<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->



<!--Ads and Related Buttons--><!-- Ads minus related Buttons -->
 
Back
Top Bottom