MALAWI has now become Africa's Shining Star!!!

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
..kwanza walikuwa na utawala wa mabavu chini ya Kamuzu Banda.

..lakini kitu cha kupigiwa mfano waliendesha harakati za kisiasa za kumtoa Banda bila kulazimisha civil war.

..pia wameendesha uchaguzi mzuri mara mbili sasa, na kila wanapobadilisha uongozi wanaweka mtu makini zaidi.

..MALAWI ni landlocked na haina rasilimali kubwa ya madini. lakini wamewekeza kwenye KILIMO na sasa kuna GREEN REVOLUTION huko.

..najua wengi mumeeleza macho na masikio Rwanda na Botswana, lakini kwa kweli kama kuna nchi Watanzania tunapaswa kuwasoma kwa umakini nadhani ni MALAWI.


 
tukiiondoa CCM we can move even more than Malawi, tatizo ni CCM.
 
It is all about leadership. Sisi si tumeamua kuwa mafisadi na wapiga soga. Hatuna wa kumlaumu isipokuwa tujilaumu wenyewe. Muluzi hakuwa kiongozi mzuri. Ila huyu wa sasa anajua anachofanya na trust me, kila jirani yetu sasa anawasha indicator kutupita. Kulikoni?
 
<..pia wameendesha uchaguzi mzuri mara mbili sasa>
Jamani kwani nasi chaguzi zetu hazikuenda vizuri tokea vyama vingi kuanza?
Tatizo kidogo sio lipo Zanzibar tu ambako tunafahamu kwanini tatizo lipo? Au tunataka ndugu zetu wa Zanzibar watawaliwe tena na wamanga?
 
ngida1,

..ni kweli hata Tanzania tumeendesha chaguzi ambazo kwa kiwango kikubwa zilikuwa nzuri.

..tatizo VIONGOZI tuliowachagua ktk chaguzi hizo ni WABOVU.

..halafu mkumbuke Malawi waliathirika na ukame kama ilivyotokea Zimbabwe, lakini sasa hivi wamejikwamua na kuongeza mafuno per acre.

..kwa nchi za Kiafrika haya ndiyo maendeleo ya kweli yanayowagusa watu wengi.

..nashangaa hii habari imekuwepo muda mrefu sasa na hakuna aliyeileta hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…