Malawi na Kenya ni nchi hatari zaidi kutembea na kuendesha baiskeli

Malawi na Kenya ni nchi hatari zaidi kutembea na kuendesha baiskeli

kilam

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2011
Posts
2,092
Reaction score
2,128
Kati ya watu milioni 1.3 wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, 49% ni watu wanaotembea, waendesha baiskeli na pikipiki, shirika la mazingira la Umoja wa mataifa UNEP linasema.

Hizi ndizo takwimu za watu waliokufa wakitembea au wanapoendesha baiskeli katika ajali za barabarani:

  • Malawi: 49% wanaotembea, 14-17% wanaoendesha baiskeli
  • Kenya: 47% wanaotembea, 14% wanaoendesha baiskeli
  • Afrika kusini: 50% wanaotembea, 3% wanaoendesha baiskeli.
UNEP linasema uwekezaji wa dharura unahitajika kuimarisha miundo mbinu ya kutembea na kuendesha baiskeli ili kuokoa maisha ya mamilioni ya watu.

Ripoti ya utafiti huo wa UNEP iliyopewa jina 'Global Outlook on Walking and Cycling', inaeleza kuwa ukosefu wa uwekezaji katika kuhakikisha watu wanatembea na kuendesha baiskeli salama ndiyo unaochangia vifo vya mamilioni ya watu na kupuuza nafasi nzuri ya kuchangia katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Malawi na Kenya ni nchi hatari zaidi kutembea na kuendesha baiskeli - BBC Swahili
 
kwahivyo tz wanaokufa wengi wanakufa ndani ya gari ikigonga gari nyengine...

na kenya 39% wakakufa kwa ajali ya gari kwa gari,, 47% wanakufa kwa kugongwa na gari, na 14% ni wanaoendesha baiskeli....


hivyo ndo inamaanisha
 
Back
Top Bottom