Malawi yahalalisha matumizi ya bangi

Malawi yahalalisha matumizi ya bangi

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
8,926
Reaction score
17,880
Malawi imekua nchi ya hivi karibuni iliyoko Kusini mwa Afrika kuhalalisha kisheria ukulima na uuzaji wa ndani na nje wa bangi.

Wanaotumia bangi kama kiburudisho wanaiona bangi kama , "Malawi Gold", yaani Thahabu ya Malawi kama wanavyoiita wenyewe, kuwa moja ya dawa nzuri.

Lakini maafisa wamezuwia matumizi ya kisheria ya bangi kwa mtu binafsi.

Itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.

Mauzo ya bangi yanaweza kuchukua nafasi ya biashara ya tumbaku, ambayo inategemewa sana na Malawi.

Nchi nyingine za Afrika zilizolegeza sheria juu ya ukulima wa mmea wa bangi ni pamoja na Afrika Kusini, Zambia, Lesotho na Zimbabwe

Nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa.

Lesotho
Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo. Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho

Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini

Afrika Kusini
Nchini Afrika Kusini Mahakama ya kikatiba nchini Afrika kusini ilihalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha mwaka 2018.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kuima kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.

Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi walisheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''. Hata hivyo ni haramu kutumia bangi katika maeneo ya Umma au kuiuza.

Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini lilifurahia uhalalishwaji wa matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho.

Ghana

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .

kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatamithilika

Pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.

Korea Kaskazini

Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.

Wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.

Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapigwa bao la kiuchumi tukiwa tumesimama
 
Malawi sasa ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazoikubali bangi kisheria
Kaya.jpg

Nchini Malawi bangi itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.

Malawi imekua nchi ya hivi karibuni iliyoko Kusini mwa Afrika kuhalalisha kisheria ukulima na uuzaji wa ndani na nje wa bangi.

Wanaotumia bangi kama kiburudisho wanaiona bangi kama , "Malawi Gold", yaani Thahabu ya Malawi kama wanavyoiita wenyewe, kuwa moja ya dawa nzuri.

Lakini maafisa wamezuwia matumizi ya kisheria ya bangi kwa mtu binafsi.
1582892507243.png

Itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.

Mauzo ya bangi yanaweza kuchukua nafasi ya biashara ya tumbaku, ambayo inategemewa sana na Malawi.

Nchi nyingine za Afrika zilizolegeza sheria juu ya ukulima wa mmea wa bangi ni pamoja na Afrika Kusini, Zambia, Lesotho na Zimbabwe

Nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa.

Lesotho

Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo. Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.
1582892590539.png

Maeneo ya nyanda zaa juu ya Lesotho yana udongo wenye rutuba unaofaa kwa kilimo cha bangi
Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini

Nchini Afrika Kusini Mahakama ya kikatiba nchini Afrika kusini ilihalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha mwaka 2018.
1582892687862.png

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kuima kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.

Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi walisheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''. Hata hivyo ni haramu kutumia bangi katika maeneo ya Umma au kuiuza.

Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini lilifurahia uhalalishwaji wa matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho.

Ghana

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .
1582892753737.png
kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.

pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.

Korea Kaskazini
Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.

wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.

Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho

Chanzo: BBC
 
Nchi ya hivi karibuni kuruhusu kilimo cha bangi ni Malawi ambayo leo hii muswada wa kuruhusu kilimo hicho umepitishwa rasmi. Zambia ilikwisha ruhusu kitambo.

Jana tulishuhudia wananchi wa mkoa wa Geita wakinyang'anywa ardhi waliyopewa baada kutumia kulima bangi.

Endapo mambo yataendelea hivi kwa watu kuendelea kulima kwa kificho na nchi jirani kuendelea kuruhusu kilimo cha bangi, je serikali yetu itasalimu amri na kuruhusu kilimo cha bangi?
 
Malawi imekua nchi ya hivi karibuni iliyoko Kusini mwa Afrika kuhalalisha kisheria ukulima na uuzaji wa ndani na nje wa bangi.

Wanaotumia bangi kama kiburudisho wanaiona bangi kama , "Malawi Gold", yaani Thahabu ya Malawi kama wanavyoiita wenyewe, kuwa moja ya dawa nzuri.

Lakini maafisa wamezuwia matumizi ya kisheria ya bangi kwa mtu binafsi.

Itatumiwa kutengeneza dawa na vitambaa vya nguvu, mafuta yatokanayo na mimea, karatasi na bidhaa nyingine.

Mauzo ya bangi yanaweza kuchukua nafasi ya biashara ya tumbaku, ambayo inategemewa sana na Malawi.

Nchi nyingine za Afrika zilizolegeza sheria juu ya ukulima wa mmea wa bangi ni pamoja na Afrika Kusini, Zambia, Lesotho na Zimbabwe

Nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa.

Lesotho
Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo. Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho

Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini

Afrika Kusini
Nchini Afrika Kusini Mahakama ya kikatiba nchini Afrika kusini ilihalalisha utumiaji wa bangi kwa watu wazima katika maeneo faragha mwaka 2018.

Mahakama hiyo ilifikia uamuzi huo kwa kauli moja, kuruhusu watu wazima kutumia bangi wakiwa majumbani na kuima kiasi kinachoweza kutosheleza mahitaji binafsi.

Wanaharakati wanaounga mkono utumiaji wa bangi walisheherekea uamuzi huo wa kihistoria wakisema ''sasa tuko huru''. Hata hivyo ni haramu kutumia bangi katika maeneo ya Umma au kuiuza.

Baraza la ukuzaji bangi nchini Afrika Kusini lilifurahia uhalalishwaji wa matumizi ya bangi na kutoa wito kwa serikali kuwaondolea mashtaka watu waliyopatikana na kileo hicho.

Ghana
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .

kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.

Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatamithilika

Pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.

Korea Kaskazini
Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.

Wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.

Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta

Sent using Jamii Forums mobile app
Badili kichwa cha habari Malawi yaruhusu KILIMO cha bangi siyo MATUMIZI ya bangi. Matumizi ya bangi kwa mtu binafsi "for recreational purposes" kujiburudisha hayajaruhusiwa Malawi bado
 
Back
Top Bottom