Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Malazi haya huwa yanalipiwa kwa siku, kitanda kinaweza kuwa €20 kwa siku. Huwasaidia sana wasafiri vijana hasa wanafunzi. Kuna huduma ya maliwato, unaoga vizuri na kupata usingizi wako mnono.
Hizi huduma huwafaa sana wale walio na migogoro kwenye ndoa. Baada ya kushindwana na mama mtoto/watoto na ameshakushitaki child support agency, mshahara unamegwa juu kwa juu, unaishia kulala kwa €20 kwa siku wakati unajipanga.
Anyway huduma hii ingewafaa sana watu wa mikoani wanaopata rufaa katika hospitali kubwa mfano Muhimbili.
Changamoto za kutoa huduma hii ni pale unapopata wageni wenye kunguni, maana watasambaa chumba kizima. Changamoto ya pili ni kuweka mahasimu wawili chumba kimoja, wanaweza kuchomana visu usiku.