Malecela angeukwaa urais ingekuwaje?

Wewe unaonaje, Malecela akiwa rais, Anne first lady, Tanzania without mafisadi is possible.

mhh hii itakuwa nchi ya kusadikika, inamaana FM ES naye atateuliwa kuwa balozi wa kudumu wa Nchi ya kusadikika huko UN? Nauliza tu....
 

45 Years ago, Kibaki and Michuki were in cabinet, and Kennedy was running for president. Obama was 1 year old. 45 years later kibaki and Michuki are still in cabinet, and Obama is a president as Kennedy was. In 45 yrs Obama's father is dead, USA had different presidents in between Johnson, Carter, Nixon, Ford,Reagan,Clinton, Bush snr and jnr, but in Kenya the same guys in their 70's and 80's are still trying to tell kenyans they can make development models that work. This makes you thinks there is something wrong with Africa.

Kwa mawazo ya kumrudisha Malecela Madarakani ni sawa na kituko hicho hapo juu.
 
Inawezekana asingekuwa kiongozi mzuri sana na angeweza kuyumbishwa na haya matatizo ya migomo kama huyu Kikwete anavyoyumbishwa kama yangetokea. Hata hivyo nikimlinganisha na Kikwete ninadhani kuwa Malecela angetatua matatizo mengi kuliko ambayo yangemshinda, na huenda hata hiyo migomo isingekuwapo kabisa na hivyo asingefikia hatua ya kuchukua uamauzi huo usio wa maana.
 
CCM ina credibility ya kuongoza ikiwa na viongozi wanaopepesuka kama huyu. Wakisapotiwa na upinzani.

Mwenyewe Kitila wa Chadema keshamkubali, mambo mswano duh, Melecela for president 2010.[/B]


Itakuwa sawa na ndoto za rafiki yangu Alnacha.
 
Ha this is very interesting. Lakini ikumbukwe kuwa mwalimu alimuita Melecela mhun kutokana na issue ya Tanganyika, na nyingine ndogondogo. Nadhani kama angekuwa rais angekuwa na judgment nzuri zaidi na mwelekeo wa nchi kwa ujumla ungekuwa unaeleweka kuliko kama ilivyosasa kwenye mika hii miwili mitatu. Lakini naona tumeingia kwenye era mpya ya uongozi. Ni ndoto sana kwa CCM asili kurudi madarakani, hata JK akiondoka itakuja kadre mpya, lazima tuweze kudeal na challenges ili tuweze kwenda mbele na sio kurudi kulekule tulikotoka.
 
Angekuwa na maauzi ya busara zaidi na si ya zimamoto tunayoyaona sasa
 
Hakuna ambaye amewahi kuwa WAZIRI MKUU Nchi hii kisha akawa RAIS isipokuwa MWALIMU peke yake. Uwaziri Mkuu unawachafua wengi.
 

Duh, inaelekea CCM inautaratibu wakuitana wahuni! Aliyeitwa mhuni na Mwalimu na yeye anapata nguvu ya kuwaita watu wahuni...Dah
 
Malecela si ndiye huyu aliyewaaambia watanzania "they can go to hell"?

Mkuu Pundit,naomba nifanyie clarifications za hii statement hapo juu huyu mzee aliyasema haya lini tena?Au ndio mnataka kumwamsha FM ES atoke huko alipojificha!
 

Asante Sana Mkuu Kwa Hizi Busara!
 
Malecela angekuwa Rais watu wasingepata vyeo kwa misingi ya UANAMTANDAO au UDINI na JUU ya yote leo hii Jeetu Patel asingepandishwa kizimbani kwa kesi ya EPA!!!
 
Malecela si ndiye huyu aliyewaaambia watanzania "they can go to hell"?

Mkuu Pundit,naomba nifanyie clarifications za hii statement hapo juu huyu mzee aliyasema haya lini tena?Au ndio mnataka kumwamsha FM ES atoke huko alipojificha!

Angewapa hizi!
Richmond....go to hell, EPA...go to hell, Twin tower...go to hell,Rada...go to hell, wakati huo yuko njwiiii kwa ka wisky alikopewa na honey Annie
 
Mahojiano ya wana habari na jsm yalikuwa ya kusaidia kuweka msimamo wa dola yetu, mzee alikuwa wazi kuwa hali hairuhusu na sababu ziko wazi hivyo yeye anashauri ujumbe huu uwafikie wananchi wote na si wanafunzi tu ila hakuchelea kuwang'ata vijana wenzetu, waelewe kuwa fursa ile ni ya wote, wao kama viongozi walitarajia hoja za kisomi na majibu ya kisomi toka pande zote mbili lakini pasipo kupuuza msingi ambao ni vijana waendelee kupiga shule huku wakijadiliana na serikali na siyo kugoma kwa jambo lililowazi kuwa si mwaka huu au mwakani litakuwa.

Alijitahidi kuipa tafu serikali na kukemea ufinyu wa kufikiri wa vijana wetu ktk mambo muhimu ya kisera.

It was nice, powerful and leading............
 
Malecela si ndiye huyu aliyewaaambia watanzania "they can go to hell"?

Mkuu Pundit,naomba nifanyie clarifications za hii statement hapo juu huyu mzee aliyasema haya lini tena?Au ndio mnataka kumwamsha FM ES atoke huko alipojificha!

AmaniGK,
Hiyo hata mie naikumbuka. Nilikuwa Arusha miaka hiyo. Ilikuwa ni kati ya mwaka 1986 - 1989. Sikumbuki mwaka hasa lini. Watu (wandishi wa habari?) walimfuata Malecela na kumwuuliza matatizo ya usafiri Tanzania. Wakati huo reli ya kazi ilikuwa ni kawaida kusikia ajali mbaya imetokea. Ajali za mabasi nazo zikawa kawaida tu. Kwenye train ukisafiri ni kizaa zaa tupu. Nakumbuka safari moja miaka hiyo nilisafiri kwa Train na nilisimama kutoka Tabora mjini (saa tatu asubuhi) na nilikuja kaa kwa kama dakika 5 station ya Gairo nilivyotokea dirishani na kwenda punguza maji. Hii ni shida moja tu na niseme ilikuwa ina nafuu sana kulingana na nyingne kibao ambazo train lilikuwa linakaa hata wiki nzima njiani. Sijui ni watoto wa kike wangapi waliharibiwa kwa kukosa senti/chakula katika maeneo ya ugeni.
Walipomfuata MALECELA na kumwambia TANZANIA kuna shida ya usafiri, malecela akajibu kwa kusema " ...Nani anasema Tz kuna shida ya usafiri? Anayesema Tz kuna shida ya usafiri - HE CAN GO TO HELL......." Baada ya hapo magazeti yote yakawa yakidai AOMBE MSAMAHA. Wakasema kama yeye anasafiria Benz si kuwa wote wana uwezo huo. Mwisho walikuja wakasema "ameomba msamaha" na mjadala ukafungwa. Kama sikosei Lusekelo alikuja akaandika kuwa "inatosha awaulize Wagogo wake jinsi wanavyosafiri".
Kama kuna OLD SCHOOL ningependekeza agombee basi ni SALLIM AS. Ila hata naye ningelitaka kujua Biashara zake zikoje kwa sasa na akishika madaraka tusije kuwa tumeifanya hiyo kampuni iwe ya TAIFA.
 
Inaelekea yeye ndio atakayeyaweza kuyashughukilia matatizo yanaiyoikumba nchi ikiwemo ufisadi?

Je ni wakati wa CCM kumfikiria kama mgombea urais kwa tiketi ya chama chao 2010.[/QUOTE
J Malechela hafai hata ukatibu kata
 

Toa darasa mwanangu, kuna younguns ndiyo walikuwa wanazaliwa miaka hiyo, na wengine walikuwa vidudu etc kwa hiyo si ajabu kama hawafahamu hizo kejeli.

Malecela, Msuya na Mramba washukuru ni wanansiasa Tanzania, nchi isiyo na scutiny kwa kauli za viongozi, ama sivyo wangeshatemwa siku nyingi tu.
 
AmaniGK,
Kama kuna OLD SCHOOL ningependekeza agombee basi ni SALLIM AS. Ila hata naye ningelitaka kujua Biashara zake zikoje kwa sasa na akishika madaraka tusije kuwa tumeifanya hiyo kampuni iwe ya TAIFA.

Sidhani kwamba SAS anamiliki biashara ama kampuni inayoweza kusababisha aonekane hafai kuwa kiongozi! Mzee huyu ni nambari wani kwa uadilifu! Anazo kumbukumbu za kila senti anayopokea/inayoingia/inakotoka na anayotumia/inayotoka/inakokwenda. Kuna binadamu waadilifu Tanzania hii, bwana. Tatizo Tanzania wenye macho ya kuona na kutambua 'almasi' ni wachache!

Malecela uzoefu wa uongozi anao na anaweza kuutumia hata sasa kwa manufaa ya taifa letu hata kama yeye si rais, kama alivyofanya Mwalimu baada ya kustaafu. Aidha, wapo vijana wenye uwezo na uchungu wa dhati wa taifa letu wanaoweze kuchota busara kutoka kwa wazee hawa na nchi ikaendeshwa barabara. Mradi vijana wakubali na wawe radhi kuelewa kwamba utu uzima dawa, na kuishi kwingi ni kuona na kujifunza mengi. Kutafuta ushauri wa wazee ni jambo la busara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…