Malecela avunja ukimya!

Malecela avunja ukimya!

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Posts
2,802
Reaction score
614
Kuna taarifa kwamba wakati wowote ndani ya siku mbili hizi Mzee John Malecela anatarajiwa kutoa tamko zito ambalo linaweza kutikisa nchi na Chama cha Mapinduzi (CCM). Lakini pia tamko lake linaweza kuweka mambo sawa na kutoa mwelekeo.

Tunafuatilia.
 
Last edited by a moderator:
Kuna tetesi pia mimi nitaongea na waandishi wa habari ndani ya wiki mbili zijazo.... Bado nafuatilia kama ni kweli au la.

Samahani nimeanza kwa joke ila nashawishika kuhoji kuwa hizi tetesi zimekuwa nyingi kiasi kwamba hata maana imepotea. Leta tangazo hapa ili tulifanyie kazi. Nakumbushia tu ile tetesi ya mkutano wa Zitto na Serukamba haukufanyika..... tetesi zisiwe tete.
Nakuaminia Halisi, nasubiri
 
Mzee Malecela kama kawaida yake atakuwa katikati kujaribu kuweka mambo sawa.

Huyu mzee pamoja na kufanyiwa fouls zote na CCM lakini hakupiga kelele za kuonewa.
 
Anapima upepo kama aongee au la. nadhani ameshaona kuwa mwelekeo wa mijadala itakuja kugusa maslahi yake siku zi nyingi zijazo. Acha waendelee kubomoana
 
Kuna tetesi pia mimi nitaongea na waandishi wa habari ndani ya wiki mbili zijazo.... Bado nafuatilia kama ni kweli au la.

Samahani nimeanza kwa joke ila nashawishika kuhoji kuwa hizi tetesi zimekuwa nyingi kiasi kwamba hata maana imepotea. Leta tangazo hapa ili tulifanyie kazi. Nakumbushia tu ile tetesi ya mkutano wa Zitto na Serukamba haukufanyika..... tetesi zisiwe tete.
Nakuaminia Halisi, nasubiri
Kwi kwi kwi! Msanii ndani ya nyumba ya sanaa! loh.
Kweli mkuu sasa tunaishi kwa tetesi nyingi.
 
Nasikia harufu ya kuanguka kwa Jumanne a.k.a John Malecela, mzee upande wowote atakao simama utamlipukia tu. Kwanza kambi yake ni kambi pinzani na mtandao hivyo akisema lolote kuwakosoa watampoteza tena safari hii bila huruma maana jamaa wamejeruhiwa na mai waifu wake. na akijaribu kuwabeba na kujipendekeza wananchi watamtosa bila huruma amuulize Zitto. Kwa sasa watalaam wa kupima upepo huwa kimya na kujifanya wapo busy na mambo ya kimataifa (wapi Salim).

Mzee funika kombe mwanaharamu apite siasa hizi za leo ni WIZI MTUPU
 
Laiti wote wangesema. Sisi tungefaidi sana kwani ingetuwezesha kujua yupi yuko nasi. Lakini kwa hali ilivyo sasa wanabakia kutuaminisha kuwa wote wanajitahidi kufisadi maslahi ya Wananchi!!
 
hatakuwa na jipy sana la kututisha, kakuna mwelekeo wowote utakaojitokeza kwa taifa hili kutoka kwake,
anyway nasubiri
 
Mzee Malecela kama kawaida yake atakuwa katikati kujaribu kuweka mambo sawa.

Huyu mzee pamoja na kufanyiwa fouls zote na CCM lakini hakupiga kelele za kuonewa.

Mtanzania, Malecela ni Mgogo. Ili uweze kuishi Dodoma, inabidi uwe Mvumilivu sana. Wagoggo AKA AGWE, wana kauvimilivu sana. Wao huwa hawana maneno maneno kama sisi/nyinyi. Hata wakoloni hapo walipita tu bila kupata matatizo yoyote. Ukichunguza sana unakubali kuwa Wagogo ni Wazaramo walioenda Dodoma kuchukua Mbuzi wa Arobaini........ mengine yatakuja endelea.
 
Malecela ni yule aliyewahi kubadili jina na kuitwa jumanne akapewa magari zaidi ya 64 kwa ajili ya kampeni na waarabu. nakumbuka nyerere alimwambia John ukisha kuwa raisi utalipajie hiyo mali. Mwalimu akamwambia Ali akimpitisha Jumanne atampigia mrema debe.
CCM ni dampo kweli hata aongee nani dampo limeoza linatoa funza hakuna wa kumsikiliza.Hana jipya ana hasira ya kunyimwa ulaji yeye na kilango.
 
Laiti wote wangesema. Sisi tungefaidi sana kwani ingetuwezesha kujua yupi yuko nasi. Lakini kwa hali ilivyo sasa wanabakia kutuaminisha kuwa wote wanajitahidi kufisadi maslahi ya Wananchi!!

Kwenye siasa kama hujiamini sana fuata upepo, utakuwa salama. Ila matatizo ya kufuata upepo huwezi kufanya jambo lolote la maana kwenye jamii. Mambo mengi ya maana yanakuwa controversial mwanzoni na faida huonekana baadaye. Ukitaka usimamie wananchi kujiletea maendeleo, wananchi watachukia, ingawaje baadaye wakiona maendeleo yaliyoletwa na nguvu zao wenyewe wanaanza kufurahi.
 
Ngoja tusubiri tu maana hali ya nchi si shwari kabisa. Inafurahisha kuona ndani ya chama tawala kuna makundi ambayo at the end wananchi ndio watafaidika na mfarakano wao. Tuvumilie watoane macho wenyewe kwanza. Kila kitu huwa kina mwanzo na mwisho, hivyo inaonekana mwisho wa watu wachache kuifaidi nchi hii unafikia ukingoni(ufisadi).
 
Kuna taarifa kwamba wakati wowote ndani ya siku mbili hizi Mzee John Malecela anatarajiwa kutoa tamko zito ambalo linaweza kutikisa nchi na Chama cha Mapinduzi (CCM). Lakini pia tamko lake linaweza kuweka mambo sawa na kutoa mwelekeo.

Tunafuatilia.

Aminia, nasubiri soon itabadilika kuwa breaking news
 
Kuna tetesi pia mimi nitaongea na waandishi wa habari ndani ya wiki mbili zijazo.... Bado nafuatilia kama ni kweli au la.

Samahani nimeanza kwa joke ila nashawishika kuhoji kuwa hizi tetesi zimekuwa nyingi kiasi kwamba hata maana imepotea. Leta tangazo hapa ili tulifanyie kazi. Nakumbushia tu ile tetesi ya mkutano wa Zitto na Serukamba haukufanyika..... tetesi zisiwe tete.
Nakuaminia Halisi, nasubiri

Tetesi RA ajivua unachama CCM
 
Si tetesi tena. Amekwisha kuzungumza na amezungumza mambo mengi. Amezungumzia nyumbani kwake Sea View saa tano asubuhi. Tutawaletea baadae. Acheni kutukana watu na uzushi wa mambo ya kampenii chafu za wakati ule. Kama kuna mtu ana hoja atafute jukwa la kuzungumzia si kumtukana mzee wa watu. Kwa sasa tusubiri kusikia alichokisema.
 
Duh sasa hivi Bongo kila mtu anajitahidi pakutokea sijui mzee atakuwa na jipya?
 
Si tetesi tena. Amekwisha kuzungumza na amezungumza mambo mengi. Amezungumzia nyumbani kwake Sea View saa tano asubuhi. Tutawaletea baadae. Acheni kutukana watu na uzushi wa mambo ya kampenii chafu za wakati ule. Kama kuna mtu ana hoja atafute jukwa la kuzungumzia si kumtukana mzee wa watu. Kwa sasa tusubiri kusikia alichokisema.

...nilishasema nakuaminia.
thanx kwa info
am waiting kupata nondo
 
mambo ya siasa hayo.kwa hiyo tumeyazoea hasa inapofikia kipindi cha kujinandi kuomba kura tena ukizingatia uchaguzi 2010
 
mambo ya siasa hayo.kwa hiyo tumeyazoea hasa inapofikia kipindi cha kujinandi kuomba kura tena ukizingatia uchaguzi 2010

itakuwa kioja cha mwaka endapo malecela akaamua kugombea ubunge tena...
au ni tetesi tu?
 
Back
Top Bottom