- Huwezi kuelimika kama huwezi kukubali kuwa huna elimu ya kutosha, nimekubali kuwa mkuu una elimu kubwa sana na upeo mkubwa, sasa kushindwa kwako kuliona hili ni moja ya mapungufu yako aynayosababishwa na jazba na ukali wako, katika kujaribu ku-intimdate mtu unayetaka kunifundisha ndio maana huwezi kumuelimisha mtu wa namna yangu ambaye ni intimdated tayari kutokana na jazba na ukali wako.
Ona vipande vya watu walioelimika hao, lakini kadiri walivyoelimika zaidi ndivyo walivyoelimika kwamba hawajaelimika
Newton
"I was like a boy playing on the sea-shore, and diverting myself now and then finding a smoother pebble or a prettier shell than ordinary, whilst the great ocean of truth lay all undiscovered before me."
"If I have seen further than others, it is by standing upon the shoulders of giants."
Kwa hiyo bin adam hajaelimika, na akielimika kidogo, kadiri anavyoelimika ndivyo anavyojua zaidi kwamba hajaelimika.
Kuhusu ku intimidate na jazba nimeshaongea.Unanikumbusha wale vijana wa Taifa Stars walioleta malalamiko yao, wako sensitive kiasi kocha akitoa discipline wanashindwa kunywa kidonge kichungu na kuchukua somo wanaona wamekosewa staha.Wewe umeelezwa ulichokosea unaona watu wana jazba na wakali, wamekukosea heshima, si hivyo, bora unakosolewa hapa JF nyumbani, kesho keshokutwa utakuwa kwenye hadhira isiyojua chochote kuhusu wewe yukasema kitu sawa na "legally alikuwa mbunge from a to b" either uka mu implicate mtu legally au ukaonekana mahamume.
- Zero tolerance huku ukiwa una-deal na hoja za wengine bin-adam wenye mapungufu kama wewe? Eti umasikini wetu wa-Tanzania unatokana na ku-tolerate kauli tata za wananchi wengine? Mkuu kumbe na wewe mtupu? Eti unakuwa zero tolerance lakini unaambilika?
Naam, bin-adam kwa kuwa sote tuna mapungufu basi tunahitajiana zaidi kuelekezana katika kila jambo.Na mie nimo humo humo, sina maana ya kwamba usinikosoe, utakuwa hunitendei haki kama utaijua njia lakini hutanionyesha, na utaweza hata kukosa thawabu yako ya kunionyesha njia.
Umaskini wetu unatokana na Mengi, mojawapo ni hili la kutokuwa na upembuzi yakinifu wa fikra na kauli, kama macho ni mlango wa kuingia kwenye nafsi basi kauli ni mlango wa kuona fikra za mtu, ukitaka kujua mtu anafikiri vipi msikize anavyosema na soma anavyoandika. Kama hatuna tabia ya kuwa precise katika maneno basi hiyo ina maana hatuna mawazo precise, na kutoka hapo hata matendo yetu yatayumba. Kwa hiyo, kwa sababu hatuna "zero tolerance" wanasiasa wetu wanatudanganya tu, waandishi wetu wanatudanganya tu (Malecela amekuwa mbunge wa Mtera kwa miaka 40) na sisi wenyewe tunadanganyana tu, ili mradi shaghalabaghala.
Naam, zero tolerance inahitajika sana.Tunapokemea ufisadi na rushwa tunatumia zero tolerance, kwa sababu tungeweza kusema "ndiyo style yetu, waacheni wale".Kwa hiyo hizi principle za "zero tolerance" zinatakiwa hata kwenye mawazo na kauli yetu.
- Zero tolerance katika mijadala na wananchi wenzio huoni kuwa hapa sio mahali pake mpaka nikuambie? Unafikiri wote hapa tuna elimu saawa na upeo sawa mkuu? Sasa bado huoni the misplace of your big words?
Ukifikiri zero tolerance inabidi tumuwekee Rostam Aziz na mafisadi tu huoni kuwa utakuwa unatumia "double standards"? Naona "conflict of interest" imekuingia umekuwa makini sana, weka umakini huo huo katika concept ya "double standards", principe yoyote unayotaka kui apply kwa fisadi uweze kui apply kwako mwenyewe.
Ni kwa sababu wote hatuna elimu ya sawa ndiyo maana tunahitajiana kuelimishana, na hakuna flow ya ideas kwamba ni lazima huyu amuelimishe huyu, hata darasani mara nyingine mwalimu anafundishwa na wanafunzi wake.
Big words nimeshakuambia unionyeshe ni wapi, pengine ni changamoto kwako ku build up your vocab vile vile.
- Ya illegally, sikuyasema ila nimesema ya legally, unakuwaje mbunge legally kama huwezi hudhuria vikao vya wabunge nje ya bunge? Na huwezi kuitwa mbunge?
Ukiyataja ya legally umeyataja ya illegally by induction, hizi ni pande mbili za sarafu ile ile.
Tanzania tuna watu wabunge, na wengine si wabunge, hatuna wabunge legal, kuwa mbunge maana yake ni kwamba uko legal kwa hiyo mbunge legal ni an unnecessary and confusing misnomer.
Either mbunge, au si mbunge.Ukitaka kumleta mbunge legal basi hapo hapo umemuonyesha kwamba anawezekana kuwepo mbunge illegal.
William.