Ugeni si kitu chema, Mpoto ndoalosema,
Pema usijapo pema,JF hakika ni pema,
Mimi mwingi wa hekima,nina mengi ya kusema,
Mstakabali ndo jina langu,nipokeeni wenzangu.
usimfuate mpoto, upotoke kama foto,
miguu kama ufito, ewe malenga mtoto,
mizani gongo la mboto, na vina kwako ni ndoto,
hekima kitu adhimu, tutakupa tukipenda!
Wewe hunayo hekima, kisa umejiunga nasi
jitofautishe na kima, uyamenye mananasi,
vitani sikae nyuma, kwenye milio ya risasi
hekima kitu adhimu, tutakupa tukipenda.
Piga ngoma na kucheza, hii uliona wapi,
kiwete hawi mcheza, yeye bingwa wa pipi
mtini acha jikweza, tavuliwa mpaka chopi,
hekima kitu adhimu, tutakupa tukipenda,
kama kweli wewe ndiye, tusimulie kwa vina
ukiwa na kiseyeye, jei efu iko pina,
hatuchezagi uyeye, sijaribu kuguguna,
hekima hujipi wewe, jipambanue tukujue,
msikilize na
Paw, vigezo uzingatie,
kama sheria ya faw,
Invisible aipitie,
kama umezoea waw, ban
Fang sikupitie
kweli wewe mgeni, kambayo guuni sitoe.