Malenga wa Kibiti asema," Tangu paka kaondoka, panya nyumba watawala"

Malenga wa Kibiti asema," Tangu paka kaondoka, panya nyumba watawala"

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2021
Posts
3,095
Reaction score
4,632
Paka kiwepo pahala,panya hawana pirika,
Pale kakamata dola, panya wanadhoofika.
Mashimoni wanalala, kero tunapumzika.
Tangu paka kuondoka,panya nyumba watawala.

Paka walikuwa jela,kifungo walifungika,
Wakawa si wa kitala,midomo walifungika.
Kuondoka wa kuwala,jikoni ni patashika,
Tangu paka kuondoka,panya nyumba watawala.

Ameandika Hassan Msati wa Kibiti
I don't want to make a comment on this
 
Huuu ndi uchonganishi wenyewe aliozungumzia Mama Samia.
Serikali zote huwa sawa na paka ,mbele ya wahalifu.
Kwa hiyo Paka hajaondoka, Bali yule alikuwa Dume na Huyu ni Paka Jike Na paka jike ndo mzuri kwa kukaamta panya.
Kama huamini sikilizia Upepo. Mzuri wa Kuvizia na kuweka Mitego,Hana Makukuru kakara.
 
Paka walikuwa jela,kifungo walifungika,
Wakawa si wa kitala,midomo walifungika.


Kweli paka alikuwa jela na hata sasa yupo jela ya milele, na panya anafuraha tele.

I had to comment on this verse.
 
Back
Top Bottom