Maramla
JF-Expert Member
- Jan 8, 2014
- 588
- 648
Hii inapatikana sehemu ya 3 ibara ya 13 (1-2) na nukuu
13-(1) lengo la katiba hii kiuchumi ni kujenga uchumi wa kisasa utakaowezesha wananchi na taifa kujitegemea kwa kuzingatia matumizi ya elimu ya sayansi na teknolojia katika nyanja zote za uzalishaji mali kwa kuhimiza mapinduzi ya kilimo,ufugaji na uvuvi, mapinduzi ya viwanda na kujenga sekta muhimu ya nishati,mawasiliano na miundombinu.
(2) Katika kuhakikisha utekelezaji wa lengo hilo , serikali itachukua hatua zifuatazo
(a)kiweka na kutekeleza mpango mkakati wa kutoa elimu ya kisasa yenye kusisitiza ubunifu, sayansi na teknolojia kuanzia ngazi ya msingi,sekondari ufundi na amali hadi vyuo vikuu na katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya taifa kwa ujumla;
(b)kuimarisha na kujenga uwezo wa vyama vya ushirika ili viwe vyombo madhubuti vya kueneza taarifa, mbinu na zana bora za kisasa katika kilimo,ufugaji na uvuvi ili kuongeza tija katika uzalishaji, kutoa mikopo,kutafuta na kuendeleza masoko
(c)kuweka utaratibu wa kujenga viwanda mama, viwanda vya kati na viwanda vidogo vitakavyosindika na kuchakata bidhaa za kilimo, ufugaji, uvuvi na madini ili kuziongezea thamani kwa ajili ya mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi;
(d)kuhakikisha kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanakuwa na ardhi na nyenzo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao katika kukuza mazingira yaliyobora kwa ajili ya kuhamasisha sekta binafsi katika uchumi, upangaji na usimamizi wa mizania ya bei za mazao na pembejeo;
(e)kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na kukuza fursa za uwekezaji;
(d)kuhamasisha uwekezaji wa pamoja baina ya raia na wasio raia katika miundombinu ya uchumi, uvunaji wa rasilimali na maliasili za taifa;
(g)kuhakikisha kwamba shughuli za serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo utajiri wa taifa unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote na kuweka mazingira yatakayochochea maendeleo linganifu na kuwawezesha wananchi kuondokana na umaskini; na
(h)kuweka utaratibu wa usimamizi na udhibiti wa huduma za kiuchumi na kijamii ili kuwezesha ushindani wenye haki na ubora wa viwango vya huduma zinazotolewa ili kuwalinda wananchi
N:B nategemea watu wasome iwe kama catalysts ya kuendelea kuisoma katiba inayopendekezwa...tumeongezewa muda hatuna kisingizio tena kwa muda hautoshi kuisoma.....