Malengo yangu milioni 25 kila mwaka

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Habari wana JF,

Nikiwa kama kijana ambae natafuta mafanikio kwa njia ya halali navuja jasho asubuhi machana kutwa nikitafuta mafanikio na kujenga msingi wa familia yangu waweze kuishi maisha mazuri yenye furaha ""Pesa ndio sabuni ya Roho""

Hapo hapo naendelea kufanya ibada ili nipate baraka na Neema kutoka kwa mola wangu muumba wa mbingu na ardhi ukiwa mwezi mtukufu wa Ramadhani naomba kuwatakia mfungo mwema waislam wenzangu.

Tuendelee kuupa eshima mwezi mtukufu kwani ni mwezi ambao umeshushwa Qruan ndani yake.

Nisiwachoshe sana naomba niingie kwenye mada husika.

Kwasasa nafanya biashara ya Duka la Jumla bidhaa kama Tambi mafuta ya kura sababu nk...najua wengi wanaelewa nature ya Duka la Jumla.

Mapema mwanzoni mwaka jana nikapata wazo la kujiwekea wakiba kwani ""NdoNdo si Chururu"

Nikapata wazo la kujiwekea 27,500 kila siku 27,500[emoji808]365 = 10,037,500 ndani ya mwaka 2017 nikafanikiwa kuweza kupata milion 10 hii ilinipa hamasa na kunipa ujasiri mkubwa.

Lakini Target yangu kwa mwaka niweze kuingiza 25 milioni naomba ushauri wenu wana JF.

Ahsanteni
 
Acha kutuchora mkuuu,,kama umeweza kujua Kwa mwaka umeingiza 10m sasa unataka kuingza 25 inamana unashindwa kujua ufanye saving ya shingap?au unatuchora
 
Fanya cross multiplication hapo....
 
Mkuu ingia kwenye football betting,tafuta odds 3 sure,tia hiyo m10,ukiamka una m30
 
Hongera zako kuna dada humu JF hachezi mbali akisikia pesa atakuja punde.
 
Acha kutuchora mkuuu,,kama umeweza kujua Kwa mwaka umeingiza 10m sasa unataka kuingza 25 inamana unashindwa kujua ufanye saving ya shingap?au unatuchora
we jamaa unanyonya nini kwenye iyo avatar
 
Ni vizuri, ila isiwe ni kikomo...u need to go beyond that 25M. Billgates aliwahi kuwaambia maprofesa wake kwamba atakua millionaire kabla hajaturn 30 yrs, guess what! By 31 he was a billionaire
 
Maduka ya jumla ukipata sehem yenye mzunguko mkubwa yanatoa sana. Jamaa angu aliinvest 30m pale mbagala after 1yr alikua na 57.
Tangazo kidogo: Ukitaka tambi na sukari kwa bei ya Jumla njoo PM
 
Unahitaji tu PM yako ijae mda sio mrefu..nothing else
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…