SoC04 Malezi Bora, uongozi imara na mfumo wa elimu kutazamwa kwa jicho la tátu

SoC04 Malezi Bora, uongozi imara na mfumo wa elimu kutazamwa kwa jicho la tátu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Silver 2024

New Member
Joined
May 29, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Malezi Bora yanajumuisha wazazi wote wawili kuishi pamoja na kushirikiana.

Ili kuibadilisha Tanzania yetu ni vyema malezi ya watoto yaanze tokea mtoto anapo zaliwa. Malezi bora yanatokana na wazazi wote wawili (baba na mama) kushirikiana, kushirikiana Katka malezi ya mtoto itasaidia mtoto kukua katika mwenendo sahihi wa msingi ya wazazi ikiwemo kujua maadili mema na kukua katika msingi ya kidini.

Madhara ya mtoto kulelewa na mzazi mmoja.
1. Kuwa na uhuru kupitiliza.
Mzazi mmoja anapo achiwa mtoto amlee peke yake ni mara chache Sana mtoto Ata kuwa na pamoja na mzazi wake mara nyingi mzazi Atakuwa katika utafutaji na mtoto atabaki nyumbani na akiwa nyamban Ana uhuru kufanya chochote ama kwenda popote.

2.Nirahisi Sana mtoto kujiunga na makundi ya kihalifu, kutumia madawa ya kulevya, na kutokufanya kazi za nyumbani

3. Sio rahisi mzazi mmoja Kuwa anafuatilia maendeleo ya mtoto wake Ata akiwa shuleni pia nyumbani

4. Ni rahisi Sana mtoto anae ishi na mzazi mmoja kufanyiwa vítendo vya kitatili, kama kubakwa, na kupewa adhabu kali pindi atakapo kosea, hili ni dhairi kabisa sababu Ata mwaka huu 2024 tumeshuhudia wazazi wengi wa kiume(baba) kuwalawiti watoto wao.

5.Mzazi akibaki peke yake na watoto ni rahisi yeye kutelekeza Familia na kwenda kuanzia maisha mengine ama uyo mzazi akaamua kuoa ama kuolewa na mtu mwingne, kama atabaki na watoto na akaoa ama kuolewa ni rahisi hawa wototo kuchukiwa ama kubaguliwa na uyo mzazi wao wa kambo.

Mambo ya kufanyika ili kupata malezi mazuri ya watoto.
1. Naishauri serikali ifanyanye juu chini kuzuia ndoa za utotoni, mabinti wengi wanaopata watoto wakiwa na umri mdogo wengi wao huwa ni wanafunzi anaishi kwao hawana elimu yoyote ya malezi kwa watoto, mabinti Hao weny watoto Hutegemea wazazi wao kuwatunza wakiwa wajawazito, wakiwa uzazi na hata watoto wanapo anza shule, ambapo kimsingi hayo majukumu angetakiwa ayafanye mwanaume aliye mpa ujauzito, Lakiwa mwanaume huyo hawezi maana huishia jela.

2. Napendekeza sheria iwekwe ili kutokomeza tabia ya baadh ya mabinti kupata mimba na kutelekeza watoto ama kuwaachia wazazi wao watoto, hii tabia tabia ipo Sana vijijini yaan mabinti wanapo maliza masomo yao wengi wao hukimbilia mijini Kisha wakishapata ujauzito hurudi kujifungulia vituo vya nyumbani, na kuwapa wazazi wao majukumu Tena ya kulea

3.ili kupata jamii yenye mwenendo mzuri wa maendeleo ni vyema serikali kupitisha sheria kwa wanaotengana bílá kujali kama walifunga ndoa ama hawakufunga ndoa, Nashauri Kuwa ni vyema watu wanao ishi pamoja kama baba na mama watambulike na ofisi za vijiji ama za vitongoji ili ikitokea wakaachana, viongozi wa vijiji na vitongoji wawafuatilie ili kujua maendeleo ya watoto wao, pia wakiachana itambulike ni Nani Atakuwa na kujumu la kuwasomesha na jukumu la kuwaangalia.

4.Napendekeza sheria ya mtoto kuishi na wazazi wote wawili iwe ni lazima kama wote watakuwa Hai. Siamini kama kuna mtu aliye juu ya sheria, sheria zipo ili zisaidie watu kufuata utaratibu uliowekwa. Sasa Tanzania yangu kuna wanawake wengi Sana wanao ishi na watoto bílá baba zao, Tena unakuta mwanamke Ana watoto wanne Lakin kila mtoto ana baba yake.

5. Serikali iweke mikakati na mipango ya idadi ya watoto watakao zaliwa katika kila familia, mikakati hiyo inatakiwa iendane na uwezo wa Familia, ikiwemo fedha, malí na historia za nyuma za wazazi, hii itasaidia Sana Familia kubaki katika Hali ya Aman pindi wazazi watakapo tangulia mbele za haki pia itasaidia mtoto kuweza kusoma mpaka level za juu za elimu, nakumbuka baada ya wazazi wangu kuachana mzazi niliye baki nae Alipata mtoto mwingne kwa mtu mwingne kipindi nipo chuo, ilinibidi uniache chuo kwa sababu pesa za Ada mzazi wangu alizitumia kumlea uyo mtoto me nikawa nikidai ela za matumizi na Ada naambiwa tu hela hamna.

Uongozi imara utasadia Sana kufikia Tanzania tuitakayo.
Watoto ni taifa la kesho. Msemo huu ni maarufu Tanzania, Kuna haja kubwa sérikali kuwaandaa watoto kuwa viongozi wakiwa bado na umri mdogo, kwa kuwashirikisha wazazi, watu wa dini na waalimu, mtoto anapo andaliwa kuwa kiongozi akiwa na umri mdogo hakuna kitakacho mbadilisha Ata akiwa mkubwa, Tena mtoto Akindaliwa Akiwa bado mdogo atukuwa muajibikaji, asiye na tamaa wala ulafi wa madaraka atakuwa mchapa kazi Sana.

Faida za mtoto kufunzwa uongozi Akiwa mdogo
1.Atakuwa muajibikaji, mtoto atakuwa na uelewa wa kile kinacho stáhili kufanyika, kwa sababu atakuwa tayar amesha fundishwa

2.Atakuwa mtenda haki, sio rahisi kwa mtu kutoka katika msingi ya kile alicho fundishwa tokea akiwa mdogo maana mpaka akuwe mtu mzima na apewe uongozi atakua ametambua mema yote na mabaya yote katika uongozi

3.itapunguza changamoto ya rushwa, Rushwa ni taama za mtu binafsi, mtoto akifundishwa njia za kuridhika na atakacho kipata tokea utotoni Ata ukubwani lazima awe anaridhika maana atakuwa anayajua madhara yake tangu utotoni

4.utatuzi wa changamoto mbali mbali katika jamii kwa urahisi, mtoto atakapofika katika umri wa kupewa Madaraka utaweza kutatua changamoto nyingi maana atakuwa amesha jifunza shuleni namna ya tatatua na njia sahihi ya kuzitatua bílá watu wengine kuonewa Ama kubaguliwa

5.itasaidia kuleta viongozi wenye sera nzurii za kisiasa pia itasaidia kuleta viongozi kwenye ushindani katika taifa letu, siku hizi viongozi wengi huonekana wakat tu wa matukio na wakati wa Kampěni katika maeneo yao, hii inatokana na watu wakipewa majukumu wakiwa watu wazima wengi hushindwa namna ya kuanza kwa sababu walio waachia kíti pia hakuwajibika vyema.

Mfumo wa elimu katika nchi yetu.
Asilimia kubwa ya watu tulio soma hatufanyi kazi zinazo husiana na vitu ulivyo somea, mfano kama mtu alisomea ualimu utaweza kukuta ni askari, Kuna haja ya mwanafunzi anapo maliza elimu ya msingi aende moja kwa moja kwenye fani anayoitaka.

Mambo ya kuboresha mfumo wetu wa elimu.
1.mtaala wa elimu ubadilishwe, masomao mengine yanayo fundishwa shuleni yanamsaidia mtoto kufaulu mitiani wala sio kufaulu maisha, karatasi ya mtiani haiwezi kuamua hatma ya mwanafunzi, mimi Nina shauri mitiani ya karatasi iondolewe badala yake iwepo mitiani ya vitendo maana sio wote wanao faulu ni kwamba wanajua sana kuliko wale walio feli

2.Shule za kulala (boarding) ziwe nyingi kuliko shule za kwenda na kurudi (Day). Hilo litasaidia Sana watoto kufaulu kwa kiasi kikubwa na itasaidia kupunguza

3.Teknilojia itumike katika ufundishaji, Sasa Dunia ni kidigitali, mambo ya kutumia chaki na ubao yameshapitwa na wakati ni vyema serikali ibadilishe huo mfumo na kutumia vifaa vya kidigitali kama vile TV, microphone na project kuanzia elimu ya msingi mpaka vyuo.

4.adhabi ya viboko iondolewe mashuleni, baadh ya shule Kuna waalimu wanasifika kwa kuchapa badala wasifike kwa ufundishaji mzuri, mtoto anachapwa mpaka anashindwa kuendelea na shule ama wengine wanachapwa mpaka wanaumwa, ni vyema hii adhabu ya viboko iondolewe kwa sababu wengine huchapwa wanapo feli, ama kuchelewa shuleni bílá mwalimu kujali kitu ambacho kimesababisha mwanafunzi kufanya hivyo

5.Baadhi ya masomo kuongezwa. Napendekeza masomo mapya yaanze kufundishwa mashuleni, masomo yatakayo msaidia mwanafunzi atakapo hitimu shule aanze maisha yake bílá kutegemea ajira za serikali ambazo ajira hizo zimekuwa kama hadithi kwa kila muhitimu, masoma ya namna ya kutafuta maisha, masomo ya veta na masomo ya teknolojia yaanze kufundishwa kwa mwanafunzi wakiwa bado wadogo
 
Upvote 0
Back
Top Bottom