Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Mnamo Disemba 2 2024 , serikali ya kijeshi ya Mali inayoongozwa na Jenerali Assimi Goita ilitoa hati ya kukamatwa kwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Barrick Bwana Mark Bristow.
Mtendaji Mkuu huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo utakatishaji wa fedha pamoja na uvunjaji wa makubaliano yanayohusu malipo ya kodi.
Mwezi uliopita serikali ya Mali pia iliwakamata maafisa wengine wanne wa juu wa kampuni ya Barrick kwa tuhuma za ukwepaji kodi.Maafisa hao bado wameshikiliwa wakisubiri kupelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili
Vilevile ilimkamata afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Resolute Mining ya nchini Australia Bwana Terry Holohan kwa tuhuma kama hizo na ilimuachia baada ya kampuni hiyo kukubali kulipa faini ya Dollar milioni 160.
Chanzo/ Source: Mining Weekly