Mali za mtu aliyepotea zinaweza kugawiwa kwa njia ya mirathi

Bashir Yakub

Member
Joined
May 27, 2013
Posts
96
Reaction score
1,745
MALI ZA MTU ALIYEPOTEA ZINAWEZA KUGAWIWA KWA NJIA YA MIRATHI.

Ikiwa ndugu yako, mme, mke, mtoto, kaka, dada nk.amepotea kwa kipindi cha Miaka 7 na hakuna taarifa zozote kujua aliko, basi inaruhusiwa mali zake kugawiwa kwa njia ya mirathi.

Huu ni muongozo wa Mahakama kuu ya Tanzania katika Maombi No. 71/202. Hata hivyo hatua hii inakuja baada ya kumuazimia aliyepotea kuwa amekufa.

Maana yake sheria katika mirathi imeruhusu mtu aliyepotea kwa miaka 7 na kuendelea kumuazimia/kumtangaza kuwa amekufa. Akishatangazwa kuwa amekufa basi haki ya kuingiza mali zake katika mirathi kwa wale wanaostahili inaibuka.

Ushahidi kuwa amepotea na haijulikani alipo ni pamoja na matangazo yenye picha yake kwenye magazeti na vyombo mbalimbali vya habari. Ushanidi wa ndugu , jamaa,marafiki, wafanyakazi wenzake kama wapo nk.

Basi mali zake zikishaingizwa katika mirathi zitagawiwa kwa warithi halali kama sheria husika inavyoelekeza. Kwahiyo wenye tatizo la namna hii wanaweza kujielekeza katika utaratibu huo wa kisheria.
 
naomba kujua mgawanyiko kama aliyokufa ni mume na kaacha mke na watoto alikini hakuwa na ndoa
 
Maelezo yako yanachanganya naoma uandike vizuri.

Ameacha mke na watoto lakini hakuwa na ndoa? Huyo mke alimpataje bila ndoa
 
sawa marehemu alikuwa na mke akafanikiwa kupata watoto watatu wakaachana na akaanza kuishi na mwanamke mwingine ambaye akufunga naye ndoa lakini wameishi kwa kipindi kirefu naye wakapata watoto watatu ,sasa amefariki na kuacha mwanamke aliyekuwa anaishi naye baada ya kuchana na mke wake na watoto sita ninachotaka kufahamu ni kwamba kuna pesa za merehemu zimetoka naomba kujua zinagawanywaje kisheria kwa hawa watoto na mwanamke aliyepo
 
Ukoo wa mume unapaswa ukae kikoo na umteue msimamizi wa mirathi na kisha hiyo alieteuliwa aende mahakaman akiwa na muhtasari
 
hilo limefanyika na linaendelea lakini tatizo ni hizi fedha ambazo zimelipwa kwa marehemu ambazo mahakama inatakiwa kuwagawia wahusika yaani mama na watoto sita
 
Msimamizi wa mirathi ni nani?
 
Back
Top Bottom