Malikia Cleopatra wa Misri

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887
TUJIFUNZE YA CLEOPATRA, MALIKIA WA KEMET/EGYPT/MISIRI ANAYESADIKIKA KUWA MWANAMKE MZURI KATIKA HISTORIA YA DUNIA

Na Comred Mbwana Allyamtu .
Wednesday-11/10/2017.

Malkia Cleopatra ni maarufu zaidi kati ya malkia wote waliowahi kutawala Misri. Cleopatra alizaliwa Alexandria mwaka wa 69 K.K (kabla ya kristo),Wakati wa utawala wa familia ya Ptolemy kwenda kwa Ptolemy XII. Cleopatra lilitokea kuwa jina maarufu ndani ya familia, kwani mama yake alilipenda kiasi cha kuchukiza kwa wengine lakini pia ndiye alikua binti mkubwa. Cleopatra hakua Mmisri, isipokuwa alikuwa Macedonia familia yake ikitoka katika kipindi cha utawala wa Alexander the Great. Cleopatra alikuwa mtawala wa kwanza katika familia yake ambaye aliongea lugha halisi ya Misri.

Inasadikika kuwa huyu ndiyo mwanamke mzuri kuliko wote katika historia ya dunia. Ametajwa katika vitabu kadhaa ikiwemo Biblia na aliishi kwa miaka 39. Cleopatra alikuwa ndiyo mtawala wa mwisho wa Kigiriki kutawala Misri na ndiyo aliyekuwa Farao wa Kwanza wa kike mgeni. Alizaliwa mwaka 69 na akiwa na miaka 18 akatawazwa kuwa Malkia.

Cleopatra ni neno la Kigiriki linalomanisha "baba yangu ni maarufu" Cleopatra ni jina walilolopewa mabinti wa kifalme wa kigiriki huku wale wa kiume wa kifalme waliitwa Ptolemy.

[emoji117]NAMNA CLEOPATRA ALIVYORITHI UTAWALA WA PTOLEMY

Mfalme wa Misri, Ptolemy wa XII, anakufa mnamo mwaka wa 51 K.K. anaacha utawala kwa kijana wake mdogo mwenye miaka 12 Ptolemy XIII. Ptolemy alikuwa ni mmoja wa wale majenerali wanne wa Alexander Mkuu,ndiyo hawa waliougawa ufalme wa Alexander katika falme nne Ptolemy ndiye aliyeanzisha utawala wa Kigiriki Misri na mji wa Alexandria ndiyo ukawa makao makuu ya ufalme wake.

Lakini Ptolemy XII anaagiza kwamba, kijana huyu atawale pamoja na dada yake mkubwa, Cleopatra. Pia ni lazima amuoe, kama desturi ya utawala wa ukoo wa Ptolemy, ingawa ndoa hiyo ilikua ni kama kuigiza. ukizingatia umri wa mumewe huyo, Cleopatra alitawala yeye binafsi kama atakavyo.

Cleopatra mwenye miaka 18 mapema anathibitisha umahiri na uwezo mkuu wa kutawala, hususani katika historia ya kipindi hicho cha Medditerania. Lakini ukaribu wake na utawala wa Roma, baadae unakuja kupoteza uhuru wa Misri.

Hivyo Cleopatra huyu tunayemzungumzia hapa alikuwa ni Cleopatra wa Saba na wa mwisho. Dola la Misri lilitawaliwa na Ugiriki tangu mwaka 323 baada ya Alexander Mkuu kuishinda Misri na utawala huu uliisha mwaka 30 baada ya Cleopatra kujiua kwa kumruhusu nyoka aina ya Cobra kumgonga kifuani.

[emoji117]KISA CHA CAESAR NA CLEOPATRA 48-44 K.K

Cleopatra alikuwa na mahusiano na wanaume wengi ila wale maarufu walikuwa ni Julius Caesar na Mark Anthony huyu Caesar ndiye ambaye walizaa naye mtoto mmoja wa kiume. Baada ya kifo cha Julius Caesar mwaka 44 mapenzi yakahamia kwa Mark Anthony mnamo mwaka 42 Ili kuweza kutawala pekee yake Cleopatra alifanikiwa kuwaua wadogo zake wote,na pia aliutumia uzuri utawala wake kupata ulinzi wa kijeshi kutoka majemedari mashuhuri wa kipindi hicho.

Mathalani, kuna kipindi akiwa binti mbichi wa miaka 21 aliwaagiza watumishi wake wamviringishe kwenye zuria zuri na kulibeba kama zawadi na kulipeleka kwa Julius Caesar na pale Julius Caesar alipolifunua akakutana na Cleopatra na hapo hapo akamfanya Cleopatra mchepuko wake.

Kuwasili Kwa Julius Caesar katika mji wa Alexandria, kunampa fursa Cleopatra kuonekana Ulimwenguni kwa wakati huo. Anaachia Misri, mikononi mwa Julius Caesar ambaye baada ya kushinda vita Pompey anakua mtawala mwenye nguvu katika dola ya Roma. Julius Caesar anaamua kupumzika kati ya mwaka 47 na 7 K.K huko Misri, akimsaidia Malkia huyu hata kuangamiza majeshi ya kaka yake (ambaye hakuweza kufua dafu).

Mara baada ya Caesar kuondoka Alexandria, Cleopatra anajifungua katika majira ya Kiangazi mnamo mwaka wa 47 K.K, anadai kuwa mtoto ni wa Caesar, na pia anamfanana sana . Katika mwaka wa 46 K.K Caesar anamualika Cleopatra Roma pamoja na mwanae (ambae mara baada ya kuzaliwa alipachikwa jina Caesarion, linalo maanisha “Caesar mdogo”) ambao walikaribishwa katika jumba la kifahari likiwa na kila aina ya anasa. baadae caesar anauwawa. Baada ya Caesar kuuwawa mwaka wa 44, Cleopatra aliamua kurudi Misri na mwanae.

[emoji117]ANTONIUS NA CLEOPATRA, 41- 31 K.K

Misri ya Cleopatra bado ni utawala ambao ni huru. Lakini karibu kila sehemu ya ukanda wa Mediterrania unajihusisha na siasa za Roma na kuna uvumi umeenea Roma kwamba Cleopatra amemsaidia “Cassius, mmoja kati ya waliomuua Caesar. Katika majira ya kipupwe mnamo mwaka wa 41, Marcus Antonius anaamuru majeshi ya Roma kwenda upande wa Mashariki, na anaamuru Cleopatra aje aeleze juu ya tuhuma dhidi yake katika makao makuu yake huko Anatolia.

Cleopatra anavuka medditerania kwenda kumuona Marcus Antonius, lakini akiwa katika hali ya ujeuri, tena akiwa hana simanzi. Kambi ya Antonius iko Tarsus, maili kadhaa kwenda mto Cydnus. Malkia anawasili akiwa katika Boti ya kifahari, akiwa amevaa mavazi yakuvutia ya mahaba, yenye asili ya Kigiriki. Hazuiliki kutamanika, na mapenzi yake mara yanaangukia ndani ya nyumba ya jenerali Marcus Antonius. Cleopatra anamualika Antonius amtembelee Alexandria. Anakubali mwaliko wake kwenda Misri kumtembelea, na anawasili Alexandria wakati muafaka kwa ajili ya kupumzika wakati wa majira ya Baridi.

Baada ya Antonius kuondoka kurudi Roma, Cleopatra anajifungua mapacha, mvulana na msichana. Wanakaa muda mrefu, hadi mwaka wa 37 K.K ndipo Cleopatra na wanawe wanaungana tena na Antonius. Antonius Anamuagiza kuja Antioch, Syria ambako huko anamuoa. Sasa wanajionesha waziwazi pamoja. na wanaungana kumpinga Octavian, mpinzani mkubwa wa Antonius katika Roma.

Jenerali Antonius akiwa na jeshi lenye nguvu eneo la Mashariki, anakua na uwezo wa kumpa mkewe huyo mapokezi makubwa ya ndoa zaidi ya yale yaliokuwa mashariki ya kati (Syria). Katika desturi ya tawala nyingi za Mashariki, Cleopatra na Antonius sasa wanakua na uwezo wa kuabudu katika miungu mmoja. Katika Ugiriki wanakua “Dionysus (Antonius) na Aphrodite (Cleopatra), katika desturi za wamisri wanakua Osiris na Isis, hali kadhalika.

Makutano hayo yanafikiwa na watu wengi wanakusanyika katika Alexandria, macho yao yakiangalia yanayojili toka kwa utawala huu, Katika jukwaa kuu ameketi Antonius na Mkewe Cleopatra akiwa amevaa mavazi ya sherehe maalum mithili ya miungu wa kike wa Misri. Na katika viti vingine vinne vya kifalme wameketi watoto wao wote watatu, pamoja na yule “Caesar mdogo”, mtoto mkubwa wa Cleopatra, kwa Julius Caesar.

Mnamo majira ya jioni katika tafrija hii, ambayo baadae ilijulikana kama “harambee katika Alexandria” Antonius anaugawa utawala wa Medditerania Mashariki kwa familia yake hiyo mpya. Antonius anamtangaza Cleopatra kuwa “Malkia wa Wafalme, na “Caesar mdogo kuwa Mfalme wa Wafalme, kwa pamoja wakitawala Misri na Cyprus. na tawala zingine kwa watoto wao. Kwa Alexander, kijana wake mkubwa (umri miaka 6), anampa sehemu ya mashariki mwa Euphratia; kwa Mapacha, dada zake Alexander, Cleopatra, anawapa Libya na Tunisia, na kwa kijana wake mdogo, Ptolemy Philadelphus (miaka 2) ambaye amevaa mavazi ya kihistoria ya Macedonia, anamgawia Syria na sehemu kubwa ya Anatolia. Inakua sherehe inayovutia, lakini ambayo baadae italeta uhasama na vita.

[emoji117]VITA YA ACTIUM MWAKA 31-30 K.K

Mapigano kati ya majeshi ya Octavianus na yale ya Antonius na Cleopatra yanafanyika Actium, Ugiriki katika mwezi September. Pande zote mbili, wana majeshi makubwa ya miguu na yale ya farasi, lakini pia swala jingine ni meli za kivita za Roma, waliokuwa nazo pia. Antonius na Cleopatra wanafaida ya kuwa na meli 500, 100 zaidi ya zile za Octavianus ambazo ni 400. Hizi ni zana za mbao ambazo ni imara sana. Zikiongozwa na na jeshi mahiri linalofikia askari hadi ya 250. Antonius anapanga jeshi lake la meli, pamoja na Cleopatra na majeshi yake nyuma, hazina kubwa ya Misri, tayari kwa mapigano.

Chanzo halisi cha mapigano haya hakijulikani. Lakini Octaviunus ameenda kinyume na matakwa ya wenza hawa wa utawala wa Mashariki. Katika mapigano ya Actium meli za Octavianus zilishinda Katika hatua flani, Antonius anamjulisha Cleopatra juu ya meli zake, na mpango wakuvunja mapigano na kutoroka nae.

Antonius na Cleopatra wanafanikiwa kurudi, katika milki ya Cleopatra. Lakini wote wanaamua kujiua katika mwaka unaofuata, wakati Octavianus alipowasili Misri na Jeshi Lake. Marcus Antonius anaamua kujiua, malkia alijaribu kumshawishi kutofanya hivyo, lakini ilishindikana. Alielewa ya kwamba angepelekwa Roma na kuoneshwa kama mfungwa mbele ya halaiki. Hapa aliamua kufa tarehe 12 Agosti 30 KK.

[emoji117]KIFO CHA CLEOPATRA JUU YA “asp” NYOKA ALIEMUA CLEOPATRA 30 K.K

Cleopatra anaamua kujiua , kama ishara ya ushujaa mkubwa. Mara nyingi alichukulia “serious” uwajibikaji wake Kwa Misri. Na pia ndiyo mtawala pekee wa kutoka ukoo wake aliejifunza na kujua kuongea lugha ya Misri. Malikia anatambua kama akiwa hai tayari atakua mfungwa wa Octavianus.

Akilindwa na askari wake wachache katika sehemu ndogo ya makazi yake, anaagiza sumu ndogo ya nyoka, asp, ambayo inaingizwa kwa siri kupitia kwenye kikapu chake anachotumia kuletewa matunda. Cleopatra anavaa mavazi yake mazuri ya ki-malikia, na analala katika kiti chake cha dhahabu. anamweka “asp” katika maziwa yake. Akijitoa kafara Kwa “Amen-Re” (nyoka aina ya cobra) aliyekuwa anatambulika kama mungu wa jua wa Misri.

Anakufa kwa sumu ya nyoka huyu (asp). Muda wa mwisho wa uhai wa Malkia unakua kama “maigizo” na unakumbukwa sana katika historia ya maisha yake. Na pia anaweka kikomo cha utawala wa Ptolemy katika Misri.

Octavianus alimtafuta pia Caesarion (mwana mdogo wa Caesar) Kwa sababu aliogopa mtoto wa Caesar angekuwa hatari kwake, akamuua. Akawachukua watoto wote watatu wa Marcus Antonius, akawaonesha mbele ya halaiki ya Roma kuonesha ushindi wake. Pia anaichukua Misri kuwa sehemu ya utawala wa Roma, na kuchukua milki zote za ufalme wa Misri.

Mark Anthony na Cleopatra walijiua baada ya kushindwa kwenye vita ya Actium na Octavian Huyu Octavian ndiye mtawala alietoa amri ya Wayuhudi wote kwenda walikozaliwa wahesabiwe Sensa.

[emoji2400]Wako Mjuvi wa Historia ya dunia na mambo ya diplomasia ya dunia......
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
[emoji2398] Copy rights reserved
[emoji2400]written by Comred Mbwana Allyamtu

Email- mbwanaallyamtu990Gmail.com
 
kitabu gani kimemtaja Cleopatra katika biblia????
 
Wanasema pamoja na uzuri wake alikuwa na nguvu za ajabu - akiongea washirikina na wachawi walikuwa wakidondoka dongoka hovyo - na cha ajabu kifo chake aliumwa na nyoka Koboko. (Cobra)

 
W

weee hkn kitu km hicho
Shida moja mnasoma Bible za vichochoroni, hivi hujui royal families zinatabia ya kurithisha majina, wa kwenye makabayo ni Cleopatra Thea
 

Attachments

  • FEC1C69A-9596-4ED9-A5A7-302117A53FD4.jpeg
    365.4 KB · Views: 81
Sawa Mkuu! sasa tushike lipi? Wazungu wanasema alikuwa na asili ya Ulaya kwa urithi wa Baba yake Mfalme Ptolemy! Wa-Africa nao wanasema alikuwa mweusi na Kumbukumbu zake ziko Jumba la Maonyesho Vatican city!

Wakaendelea kusema sisi Wa-Africa tumepigwa changa la macho ili tusijejiona Bora kuliko wao, na huyu Cleopatra alitawazwa kuwa Mfalme kwa sababu alikubalika na Wa-Misri wote! ajili ya U-Africa wake na kuongea Lugha yao ya ki-Misri (Coptic) kwa ufasaha,

Hivo kufanya watu wengi wamuelewe vizuri hali amabyo ilimfanya kujenga ngome yenye jeshi Imara, iliyo kuwa tishio kwa Wazungu. Awali kabla Cleopatra hajashika madaraka ya kuiongoza Misri, familia ya Ptolemy ilitawala eneo la Alexandria tu.

Sababu kubwa kutawala kieneo kidogo cha Alexandria, ni kwamba utawala wa Ptolemy ulipingwa na weusi wengi. kutokana na kuwa

1 Magiriki .hawakuitambua, wala kutaka kutumikia miungu ya Misri km OSIRIS,

2.Pili lilikuwa Taifa la ugenini, walioonekana km wapita njia tu, siyo wakaaji,waliipenda Macedonia kulikoMisri, na wailkuwa wabaguzi wa ngoz nyeusi.

3.tatu- wazungu walitaka kuingiza miungu ya kwao yaani Olympian gods, iabidiwe nchi nzima, wamisri walipinga.

4.nne- hata Lugha ya ki-Coptic, yaani ki-Misri watawala magiriki hawakukijua. kwa sababu hii kufanya utawala uwe mgumu kwa watawala wa Falme ya Ptolemy!!

Wa-Misri wenyewe wakazuka na mwana wa misri mwenye kipaji yaani CLEOPATRA -MWA-FRICA aliye pendwa na kukubalika nchi nzima, so akaitawala Misri yote isipokuwa Alexandria (palipo kuwa Milki ya Mfalme Ptolemy),

baadaye sana wakati wakuandika historia wazungu Magiriki wakatamani hili jina maarufu lililotokea pendwa wakati wa utawala wao yaani ptolemy ktk Historia ya Misri. wakalitwaa likawa lao mpaka leo weusi hawajui!

hapa unasemajeWakabainisha kwamba Lips, macho, kipilipili, kitambaa kichwani, lips hizo pana ni za Mwafrica, Bila shaka pua pana ni Africa lkn ilitolewa maksudi, kupoteza Identity.

je kama kweli ni Mzungu mbona haina pua? Wazungu wakajibu kuwa Sanamu nyingi za MIsri ni za kale kwa hiyo ni rahisi kuharibiwa na michafuko ya hali ya hewa hali ya hewa, km Mvua, Jua kali, Upepo nk. sijui ni kweli! mpaka leo sijui nani mkweli!
 

Cleopatra ascended the throne at the age of 17 and died at the age of 39. She spoke 9 languages. She knew the language of Ancient Egypt and had learned to read hieroglyphics, a unique case in her dynasty. Apart from this, she knew Greek and the languages of the Parthians, Hebrews, Medes, Troglodytes, Syrians, Ethiopians, and Arabs.
With this knowledge, any book in the world was open to her. In addition to languages, she studied geography, history, astronomy, international diplomacy, mathematics, alchemy, medicine, zoology, economics, and other disciplines. She tried to access all the knowledge of her time.
Cleopatra spent a lot of time in a kind of ancient laboratory. She wrote some works related to herbs and cosmetics. Unfortunately, all her books were destroyed in the fire of the great Library of Alexandria in 391 AD. C. The famous physicist Galen studied her work, and was able to transcribe some of the recipes devised by Cleopatra.
One of these remedies, which Galen also recommended to her patients, was a special cream that could help bald men regain their hair. Cleopatra's books also included beauty tips, but none of them have come down to us.

The queen of Egypt was also interested in herbal healing, and thanks to her knowledge of languages she had access to numerous papyri that are lost today. Her influence on the sciences and medicine was well known in the early centuries of Christianity. She, without a doubt, is a unique figure in the history of humanity. 🇪🇬
 
Kama angekuwa mzungu mgiriki au Mroma kazi zake zinge tunzwa mpaka leo kwa vizazi na vizazi!....kuteketezwa kwa kazi za Mtawala Cleopatra na wa Roma inadhihirisha chuki za wazungu dhidi ya uafrica wake!!!

Lkn ikafika mahali wakaona huyu jinale si rahisi kufutika wakalitwaa likawa lao!! vitendo vyake vikawa vya asili yao!! lkn si kweli!!...Library kuubwa ya Misri ilichomwa moto maksudi tu!!...naa mule ndo kulikuwa na nguvu za kutawala!!!

leo hii bado waafrica wanaoenda kusoma Misri wakifika kule mizimu yao inawachukua mazimaahawarudiga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…