Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,203
- 37,906
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, ana haki zote za kuwa na urafiki na mtu na kumsapoti katika jambo lolote lenye heri. Ili mradi havunji sheria za nchi, Malinzi anaweza kwenda popote anapotaka, kuonana na yeyote anayetaka na kuzungumza na yeyote.
Lakini, kuna tofauti kubwa, kubwa sana kati ya Jamal Malinzi, kama mtu binafsi na Jamal Malinzi kama Rais wa TFF. Katika Kiswahili fasaha, tunasema tofauti ni kama kati ya mbingu na ardhi.
Nitatoa mifano michache tu. Jamal Malinzi anaweza kwenda uwanjani na kushangilia goli wakati timu yake ya Yanga inapocheza. Lakini, kama Rais wa TFF, anatakiwa kuonyesha ustahamilivu hata kama ana mapenzi binafsi.
Kama mtu binafsi, Malinzi anaweza kwenda kwenye mkutano wa vilabu akiwa amevaa fulana ya klabu anayoipenda lakini kama Rais wa TFF, kuna kiwango ambacho hawezi kuvuka kwenye kuonyesha mapenzi yake.
Kila anachofanya, anatakiwa kutanguliza kwanza maslahi ya taasisi yake kwanza kabla ya maslahi yake binafsi. Inapofika wakati wa kuchagua kati ya jambo lenye faida kwake na lenye faida kwa TFF, Rais wa TFF anatakiwa kuchagua lile lenye faida kwa taasisi.
Ni vitu vingi vidogo vidogo lakini vyenye athari kubwa, kubwa sana. Ndiyo maana, nilishangazwa na hatua yake ya kumtembelea Waziri Mkuu mstaafu juzi na kumwelekeza kuhusu mikakati ya shirikisho analoliongoza.
Swali kubwa ambalo linatakiwa kuulizwa hapa ni kwa sababu zipi Malinzi alikwenda kueleza mipango na mikakati ya TFF kwa Lowassa.
Lowassa si Waziri wa Wizara ya Habari na Michezo ambayo walau inafanya kazi kwa karibu na shirikisho hilo. Kama Lowassa angekuwa waziri wa wizara hiyo, ningeweza kuelewa lengo la Malinzi kwenda.
Kwa bahati mbaya, sijasikia kama Malinzi amewahi kwenda kwa Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Fenela Mukangara, na kumueleza kuhusu mikakati hiyo ambayo amemueleza Lowassa. Swali linarudi palepale, kwanini Malinzi alikwenda kwa mtu ambaye TFF haifanyi naye kazi moja kwa moja?
Ningemwelewa kidogo Malinzi kama Lowassa angekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambayo inajishughulisha na masuala ya michezo. Lakini Lowassa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ambayo kwa kweli haina uhusiano wa moja kwa moja na TFF.
Kama Lowassa angekuwa Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ningeweza kuelewa lengo la ziara ya Malinzi. Lakini, kwa bahati mbaya, Lowassa hajawahi kuwa mjumbe wa baraza hilo.
Niseme wazi kwamba ningeelewa kama Malinzi angekuwa amekwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete, kwa vile serikali yake ndiyo inayolipa mshahara wa Kocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars). Lakini Lowassa ni mbunge na hayuko serikalini kwa sasa.
Kama Malinzi alikuwa na shida ya kuonana na Waziri Mkuu mstaafu, yupo ambaye anafahamika kwa kupenda soka. Anaitwa Frederick Tluway Sumaye na si Edward Lowassa. Kama angekuwa amekutana na Sumaye kumweleza kuhusu mipango yake ya kuinua soka, walau ningeweza kumuelewa.
Ndiyo maana najiuliza, Malinzi alifuata nini kwa Lowassa?
Edward Ngoyai Lowassa ninayemfahamu mimi sijawahi kumuona kwenye mechi yoyote kubwa ya soka hapa nchini kwa kipindi kirefu sasa. Kimsingi, unapozungumzia majina ya wanasiasa wanaopenda mchezo wa soka, jina la Lowassa huwa halitajwi.
Tunawaona wanasiasa wanaokuja katika Uwanja wa Taifa wakati wa mechi kubwa na ndogo za mpira wa miguu. Profesa Juma Kapuya huwa anakuja uwanjani. Samuel Sitta si kwamba anahudhuria mpirani, lakini pia ni mmoja wa wadhamini wa klabu ya Simba. Nimewaona pia uwanjani, mara nyingi tu, Freeman Mbowe na Zitto Kabwe. Hawa wanapenda mpira.
Amos Makalla anakuja uwanjani. Mussa Azan Zungu anahudhuria mechi. Iddi Azzan anahudhuria mechi. Richard Ndassa anahudhuria mechi. Juma Nkamia anahudhuria mechi. Nimemwona mara nyingi Mwigulu Nchemba akihudhuria mechi katika uwanja wa Taifa ambako ndiko mechi kubwa zinapochezwa.
Sina hakika kama Lowassa amewahi kuingia kwenye uwanja huo kutazama mechi hata moja ya soka. Ni ndani kabisa ya haki yangu kusema kwamba Lowassa si mtu wa mpira. Ingekuwa hivyo, sote tungejua kwa sababu upenzi wa mpira wa miguu si jambo la kujificha. Ndiyo maana, pamoja na kushika wadhifa wa juu kabisa katika nchi hii, kila mtu anayefuatilia soka anajua kwamba Kikwete anapenda klabu ya Yanga.
Kwenye ushabiki wa soka, hakuna siri.
Lakini, jambo ambalo nimeshindwa kulielewa hadi leo ni kwamba mkoa ambao Lowassa anatoka, Arusha, una timu moja tu, tena inayomilikiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Mwaka jana, kuna baadhi ya wananchi wa Arusha walikutana kutaka kuifufua klabu maarufu zaidi ya wananchi wa mkoa huo iitwayo AFC.
Kati ya watu waliojitokeza kutaka kuikwamua timu hiyo, Lowassa hakusikika. Kabla haijashuka daraja miaka mitatu iliyopita, AFC ilikuwa miongoni mwa timu zinazoendeshwa kimasikini zaidi katika Ligi Kuu ya Tanzania kiasi kwamba ilishindwa kusafiri kwenye baadhi ya mechi za ugenini.
Arusha ndiyo jiji pekee hapa nchini ambalo halijakuwa na timu ya Ligi Kuu ya Tanzania kwa muda mrefu sasa. Mwanza ilikuwa na Toto African miaka miwili iliyopita lakini walau ilikuwepo. Sote tunajua kwamba Arusha ina watu wenye fedha na kama Lowassa angetaka, kwa kutumia ushawishi anaouonyesha kwenye kuchangisha harambee mbalimbali, AFC ingekuwa timu ya Ligi Kuu.
Tanga wana Coastal Union. Dar wana Ashanti United. Mbeya wana Mbeya City yao ingawa pia Prison ipo. Arusha, anakotoka Lowassa, haina kitu. Haina tofauti na Kigoma, Singida, Mara, Simiyu, Rukwa na mikoa mingine.
Swali linakuja tena kwa Malinzi, alikwenda kwa Lowassa kufuata nini?
Kama ningekuwa Lowassa, ningefurahia ujio wa Malinzi ofisini kwangu. Ni fursa nyingine ya kuonekana na upande ambao katika hali ya kawaida asingepata hiyo fursa. Kama huwezi kwenda mpirani, waite watu wa mpira ofisini kwako.
Sababu pekee ambayo naiona ilimsukuma Malinzi kwenda kumuona Lowassa ni ya kisiasa. Pengine Malinzi naye ameamua "kusimama ili ahesabiwe". Lakini, angeweza kufanya ziara hiyo kibinafsi na bila ya kuihusisha TFF.
Kwenye mpira hatujazoea na hatutaki siasa hizi za kibinafsi. Mpira wenyewe una siasa za kutosha kiasi kwamba hauhitaji kuingiliwa na siasa nyingine. Kama mtu anataka kufanya siasa zake, basi afanye kibinafsi na asihusishe taasisi wala wafanyakazi wake kwenye masuala hayo.
Ezekiel Kamwaga - Kaatibu SSC