serikalini mishahara ni midogo sana wote tunaishi kwa deal za kifisadi tuu siku akitokea rais makini na takukuru yenye meno magereza yote yatajaa watumishi wa serikali nasheria ya kifungo itbidi iondolewe na badala yake adhabu ya kifo iwekwe kama walivyofanya wachina hakuna sababu ya kuingia gharama kuwalisha na kuwatibu wala rushwa magerezani.malipo ya serikali yakoje wadau?
TRA Hakuna Allowances zozote zaidi ya mishahara tena haikidhi sikuizi inatofauti kidogo sana na ya watumishi wa kawaida wa serikali. watumishi wengi vijana hukimbilia taasisi zingine kutafuta ajira baada ya kupata uzoefu. Huo ndiyo ukweli wa mambo pia wamedhibitiwa sana hata rushwa hakuna siku hizi.