crome20
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 1,193
- 810
Baada ya hukumu ya miaka 3 jela kwa viongozi wa DECI na kuamuriwa kuwarudishia pesa zao wale waliopanda mbegu, mimi nawauliza wataalamu, kweli pesa hizo zinalipika? Ni utaratibu gani mahakama inauweka kuhakikisha mfungwa alieamuriwa kulipa fidia anafanya hivyo baada au akiwa bado anaendelea kutumikia adhabu ya kifungo. Swali la ziada: Hivi ni kweli kwamba siku za jela uhesabiwa asubuhi hadi jioni siku moja? na kufanya siku moja ya uraiani kuwa siku mbili za gerezani.?