Ndugu wana JF hususan walimu, napenda kufahamu malipo anayopaswa kupewa mwalimu aliyesimamia mitihani ya darasa la saba mwaka huu baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi mkuu na msimamizi wa kawaida, yaani kupewa majukumu mawili kwa wakati mmoja. Je akilipwa sawa na mwalimu aliyepewa jukumu moja ni haki? Ni sahihi kupewa kazi mbili lakini kulipwa kazi moja. Endapo jibu sio haki mwalimu huyo anastahili kuchukua hatua zipi? Nasubiri ushauri wenu wadau.