Malipo ya mabomu Mbagala: Waathirika walipwa Fidia Tshs 1,950

Malipo ya mabomu Mbagala: Waathirika walipwa Fidia Tshs 1,950

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
8,873
Reaction score
1,906
Waathirika mabomu ya Mbagala walia fidia finyu

Imeandikwa na HabariLeo

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mbele ya baadhi ya waathirika hao, Katibu wa Kamati ya Waathirika hao, Thomas Mbasha, alisema baada ya ajali hiyo, walilipwa fidia ndogo na waliandika malalamiko yao kwa njia ya maandishi kwa Serikali wakitaka kuongezwa fidia, lakini hawajapata majibu mazuri.

“Tumeandika barua kadhaa kwa Serikali tukiomba fidia zetu lakini hakuna kilichofanyika. Tunahitaji Rais aingilie kati suala hili ili tulipwe stahili zetu kabla hajaondoka madarakani,” alisema.

Mbasha alisema fidia walizolipwa awali, hazikulingana na thamani ya mali na vitu walivyopoteza wakati wa mabomu hayo.
“Inakatisha tamaa kusema haya mbele ya umma lakini ndicho tulichopewa na Sserikali kama fidia,” alisema huku akionesha nakala za hundi zikiwa na kiasi walicholipwa.

Baadhi ya hundi za malipo hayo kutoka Benki Kuu (BoT) zilikuwa za Sh 1,400; Sh 2,700; Sh 1,950 na Sh 4,900.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stephen Gimonge alisema Rais Kikwete alitembelea eneo hilo na kuahidi kuhakikisha waathirika wanalipwa fidia inayostahili lakini ahadi hiyo haijazaa matunda.

Wakizungumza na waandishi wa habari, waathirika hao waliokuwa wamekusanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mbagala Kuu, wilayani Temeke walithibitisha kupokea hundi zenye kiasi kidogo cha malipo ya fidia, huku wengine wakiandikiwa kulipwa Sh 1,000.
Omary Mbonde ambaye ni mmoja wa waathirika hao, alithibitisha kulipwa hundi ya fidia ya Sh 1,950.

“Fedha hizo nimelipwa kama fidia kwa ajili ya nyumba yangu iliyoharibika pamoja na vitu vyangu vingine,” alisema na kuongeza kuwa alipeleka malalamiko yake kwenye kamati, ili apate fidia inayostahili lakini hadi leo hajapata chochote.
 
Sisiem sisiem sisiem sisiem eeh LAzimA wanyooke nilishuhudua zakiem RAIA wanauza viparata voters id kwa ccm hay Andy malipo
 
GRHTDsbb5ni1RuLwodnHHCK2IHpge05kpjmxxDQlGfs93dxq_iYvPT7aR-63jhX6qAXdN9u0pvg3FzzWxt0AK2ESP_8-gTFMi44do7s1x-RaMJFqBPQfEBdQxksd1cNq8ezm9fnKCk2cF8GgilVZ-LAnAXBvWcbYj3xt9MRKTfFPcW--iWZ7BqanoulnLwou6pjSJJdxyv4JFEDXhYTa7pEazBgMPgYj_t0Xjb9dOf7bzDCGFA=s0-d-e1-ft

Acha iwachome ndio wanaoichagua, wacha iwacome tena na tena
 
ukombozi unahitajika Kwa kweli ccm haijali hata RAIA wake Mungu tusaidie kuwapa kiburi hicho hicho hili watu wako wafungue .macho na kupata mwanga kuiondoa madarakani ccm
 
Daaaa,kweli hii nchi imewachoka wananchi wake...hata chembe ya uhalisia haupo?...
 
Kwa hiyo hiyo hundi unaipandia daladala toka mbagala rangi 3 mpk hazina then unaenda kudeposit bank unasubiri 5 working day then unavuta mpunga.Hahahaha maisha bora kwa kila mtz.Asante baba Riz1 uko ulipo sasa hivi.
 
sasa hiyo gharama ya karatasi ya cheque ni shs ngapi? watu wana utani jamani!!!
 
Hata sahani ya bati hyo hela haitosi.

Ukute mzee wa watu ameangukiwa na nyumba nzima.
 
Gharama ya kkutengeneza hiyo karatas moja ya cheque ni zaid ya 1950 bora wangewarushia vocha ya hyo thaman kuliko huo utapel
 
Sijawaona wale vilaza wa lumumba humu,

Ritz & co mkuje huku mseme hii ni hakii?
 
Last edited by a moderator:
Sijawaona wale vilaza wa lumumba humu,

Ritz & co mkuje home mseme hii ni hakii?

Ndugu yangu ukiiwaza sana ccm utakuwa mwehu. hujui kuna waziri kapewa zawada ya 1.6 Bilioni? jiulize wangewapa milioni kumi.kila mtu wangepata wangapi? hii ndiyo Tanzania nchi yenye udongo wa dhambi
 
Last edited by a moderator:
hiyo ukideposite inayeyukia banki itakuwa ni bank charge
 
hahaha afu huyo akiambiwa ccm imechoka povu lamtoka
 
Back
Top Bottom