Analipwa mshahara kama kawaida kiwango inategemea na standard ya salon yako, unaweza fanya upelelezi ukajua kiwango wanacholipa salon za jirani.
Kuna wengine anataka akimsuka mteja rasta eg yeboyebo mnagawana pesa ya ususi nusu kwa nusu kwahiyo mshahara wake unakuwa chini na kama mapato yote yanaingia salon mshahara unakuwa juu.
Lakini kutinda nyusi unamwachia anachukua yeye. Na hapo ndipo wamiliki wa salon wanapofanya makosa makubwa kuanza salon kwa kulipa mfanyakazi mshahara mkubwa bila kujua salon itaweza kuingiza faida kiasi gani. Salon ni biashara yenye changamoto sana upande wa wafanyakazi uwe makini.