DOKEZO Malipo ya nauli za watumishi kubadilishwa matumizi Tandahimba

DOKEZO Malipo ya nauli za watumishi kubadilishwa matumizi Tandahimba

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

aliya

Member
Joined
Aug 11, 2022
Posts
20
Reaction score
14
Habari!

Napenda nielekee Moja kwa Moja kwenye mada husika!

Kuna baadhi ya halmashauri viongozi wake ni warasimu sana kitu ambacho kinashusha ari ya ufanyaji kazi kwa watumishi, mfano serikali inatoa pesa kwaajili ya nauli kwa watumishi wake ila zikifika kwenye halmashauri wanabadilisha matumizi jambo ambalo linapelekea watumishi kunyimwa stahiki zao.

Hali halisi ni halmashauri ya Tandahimba mkoa wa Mtwara hawajawahi kulipa malipo kwa wakati na hata upandishaji wa vyeo huwa wanakuwa nyuma sana, suala ambalo kimsingi halifai.

Naomba wizara ya TAMISEMI itazame kwa jicho la tatu kwenye halmashauri hii ikibidi mabadiliko yawe yanafanywa mara kwa mara, itoshe kusema mkurugenzi na wakuu wa idara ni warasimu mno.
 
Taarifa imewafikia bila ya shaka,nadhani wilaya ya Tandahimba itakuwa ina viongozi wengi wasiojielewa nàona nyuzi zimekuwa nyingi sana. Serikali angazieni macho Tandahimba kuna viongozi wanalazimisha wafungwe jela.
 
Hii nchi inabidi Rais atoe agizo la dakika moja tu tuwashughulikie viongozi wapumbavu, nadhani ingekaa poa sana
 
Hii nchi inabidi Rais atoe agizo la dakika moja tu tuwashughulikie viongozi wapumbavu, nadhani ingekaa poa sana
Si walusema walishaandaa mfumo!?? hazina si iwe inaweka tu kwenye A/c ya mtumishi moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom