Malipo ya ndege za coastal zituapo hifadhi selous

bwananyama

Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
21
Reaction score
6
Kabla ya mwaka 2009, pori la selous kanda ya utalii ya Matambwe, Ilikua ikikusanya zaidi ya 10mil kwa mwez kutoka kampuni ya ndege ya caastal, ikiwa kama landing fee.Fedha hizo zilikua zikitozwa pale pale pindi ndege zilipotoa. Lkn baada ya mwaka huo, utaratibu wa ukusanyaji fee hizo umebadilishwa. Ndege zinatua kwa mkopo, malipo mwisho wa mwezi. Cha ajabu malipo yameshuka kutoka yale ya mil10 hadi kufikia mil3 kwa mwezi (malipo yasiyo ya wazi. hulipwa dar kupitia a/c # isiyojulikana),huku trip za ndege za kampuni hyo zikiwa nying kuliko kipindi miaka kabla ya 2009! Wadau wa eneo hili either wa coastal, au watumish wa selous na wanajamvi kwa nisaidieni haya maswali 1} Ni utaratibu gan ulitumika kuondoa mfumo wa zaman wenye faida 2) Kama ni mtu binafsi kaamua kufaidika mil2 kila mwezi ashtakiwe kwa sheria gani? NAWASILISHA WAKUU.
 
Shukran mkuu kwa uzalendo wako,, nadhani wahusika wamepata pa kuanzia tatizo ni mikono ya kifisadi huku wengine tunakandamizwa na mikodi kibao ,.,.,.,..
 
Acha kupotosha watu...selous wamefunga mfumo wa kielektroniki wa kukusanya mapato hvyo utaratibu wa zamani umebadilika..wasiliana na maliasili upate taarifa rasmi ndugu
 
Acha kupotosha watu...selous wamefunga mfumo wa kielektroniki wa kukusanya mapato hvyo utaratibu wa zamani umebadilika..wasiliana na maliasili upate taarifa rasmi ndugu

Hakupotosha watu, alikuwa anatoa taarifa kwa namna anavyozifahamu yeye binafsi, na kwa nafasi aliyopo. Kama zina mapungufu basi usimlaumu ametekeleza wajibu wake kama raia mzalendo, mapungufu ya taarifa yake matokeo ya mamlaka kuhodhi taarifa na hivyo umma ukibakia ku guess nini hasa kinachoendelea.

Swali
Kwahiyo huo mfumo wa kielectronic ndio umepelekea mapato kushuka ilhali kuna ongezeko la safari za ndege kwenda Selous? Kama sikosei serikali inatumia mfumo wa Cash Basis katika ku account mapato yake, yaani malipo kwanza. Je, kwa kuwakopesha hawa watu wa coastal si kunaicheleweshea serikali mapato yanayohitajika kutekeleza mipango anuai na ni kuwapa benefit wasiyo stahili hawa watu wa Coastal?, Hilo linafanyika kwa faida ya nani???
 
Acha kupotosha watu...selous wamefunga mfumo wa kielektroniki wa kukusanya mapato hvyo utaratibu wa zamani umebadilika..wasiliana na maliasili upate taarifa rasmi ndugu

Bado kuna uwezekano mkuwa sana wa kuibiwa zaidi kwa mifumo ya kielectroniki kuliko mfumo wa zamani wa manual kwani vyote controller ni binadamu inategemea na malengo ya wahusika kuanzia configuration na hata programmer ikibidi ikitegemea na kiasi kinachlengwa ili kuibiwa mfano ma bank ndio yana mifumo ya kisasa lakini bado wanaibiwa sana. jamaa ametoa taarifa ya wazi na ni jibu la mwisho kuwa hatimaye kinachopatikana ni 3 mln badala ya 10 mln
 
Taarifa hizo ni muhimu kufanyiwa kazi maana kuna viashiria vya wizo,kuelekea 2015 tutasikia mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…