Habari zilizoandikwa katika gazeti la mwanahalisi toleo namba 207 la leo tarehe 22/9/2010 kuhusu yale malipo ya ndege ya kukodi yanatia kinyaa. Nitanukuu kwa kifupi baadhi ya sehemu muhimu. "kwenye hati ya madai ya tarehe 14 septemba mwaka huu, inayodaiwa kutolewa na mamlaka ya ndege za serikali (TGFA) kwa CCM inaonyeshwa kuwa kasma (vote) inayotawala fedha za mamlaka ni na. 062". kwa maelezo ya mwandishi huyu kasma inayotajwa haimo katika vitabu vya bajeti Vya mwaka huu wa fedha (2010/2011). Inauma sana! mwandishi amejiridhisha baada ya kufanya upekuzi wa vitabu vinne vya bajeti.
Hati zilizokaguliwa ofisini kwa kinana , mtaa wa ohio ni na.00868727 ya tarehe 31 agosti 2010 inayodai dola za kimarekani 15,000 na nyingine na. 00867909 ya tarehe 14 septemba 2010 inayodai sh. 22,950,000 zote zikionyesha kasma na. 062. Vitabu vya bajeti vilivyo pekuliwa ni
makadirio na mapato
makadirio ya matumizi ya serikali
makadirio ya matumizi ya mikoa na
makadirio ya matumizi ya maendeleo
katika vitabu vyote hivyo hakuna palipoonyeshwa kasma na. 062 ya wakala wa ndege za serikali. Habari toka wizara ya fedha ni kasma na. 1817. "Hata hivyo ofisa wa bunge aliliambia mwanahalisi kuwa kasma na.062 iliyotajwa na wakala ilikuwa katika vitabu vya bajeti vya mwaka 2006 chini ya wizara ya mawasilino na uchukuzi na kasma hiyo sasa imefutwa". KWA MAANA NYINGINE FEDHA HIZO ZINAINGIA KATIKA MIFUKO ISIYOHUSIKA.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na hivyo kuonyesha kuwa mama salma kikwete amekuwa anasafiri na hiyo ndege kama first lady na siyo mpiga kampeni wa CMM, RUBANI HUSEMA YAFUATAYO ANAPOTAKA KUTUA KIWANJANI " On board, on board, First lady, first lady!" kwa maana kwamba wamembeba mke wa raisi na siyo abiria wengine kama ilivyo zoeleka. INATIA KINYAA TUNAHITAJI USHAHIDI GANI ZAIDI WA HAYA KAMA SI UFISADI TU. NASHAURI MAMA AFUNGULIWE KESI YA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA UMMA.