Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
I’m going to go in and keep it a buck all the way.
Ni hivi, wabunge wengi sana wa bunge la Tanzania ni wachumia matumbo tu.
Hawapo bungeni kuwawakilisha wananchi wa majimbo yao.
Kwa sababu hiyo, mimi ningependa malipo yao yote, yaani kuanzia mshahara, posho zile kipumbavu, marupurupu, na mafao, yapunguzwe kwa asilimia kubwa sana. Pendekezo langu ni yapunguzwe kwa asilimia 75.
Yakipunguzwa kwa kiwango hicho, naamini hapo ndipo tutapojua nani anaenda bungeni kuwawakilisha watu wa jimboni kwake na nani anataka kwenda kwa ajili ya fursa za kiuchumi zitokanazo na ubunge.
Kwa muda mrefu sana wabunge wetu wamekuwa ni kati watumishi wa umma wanaolipwa mahela mengi sana ambayo wala hayaendani kabisa na matokeo ya kazi waifanyayo.
Hao wabunge zaidi ya kuzomeana huko bungeni na kugonga gonga meza, huwa wanafanya kazi gani inayowafanya wastahili hayo mamia ya mamilioni ya shilingi wanazolipwa?
Ifike mahali sasa malipo yao yaakisi uhalisia wa hali halisi za majimbo yao.
Yaani imefikia mahali mpaka watu wanaona kuwa kama mtu fulani hajateuliwa na chama chake kugombea kwenye jimbo fulani basi kuna kitu kilichomponza kuikosa fursa hiyo ya kujipatia mahela.
Upumbavu kabisa kutumia nafasi za uwakilishi wa wananchi kama fursa za kutoboa kiuchumi.
Ifike mahali sasa tuwe tunatumia akili kujitawala, la sivyo tutaendelea kujidanganya tu.
Punguza malipo tuone kama kutakuwepo na msururu wa watia nia.