Jana kwa kuhitimisha mjadala wa Bajeti ya Serikali 2024/25 Mhe. Waziri wa Fedha aliwahakikishia Wananchi wa Nyatwali kuwa watalipwa haraka iwezekanavyo. Malipo haya yamechelewa kwa muda wa miaka miwili na kama ilivyo sheria ya ardhi ni kuwa mwananchi usipomlipa ndani ya miezi sita tangu alipoweka sahihi yake ya thamani ya mali yake anatakiwa kulipwa nyongeza ya 7% ya thamani ya mali yake na hivyo tunakukumbusha Mhe. Waziri wa Fedha ukumbuke kuna nyongeza ya aslimia 7% katika malipo yao. Tunawashukuru Waheshimiwa Wabunge wetu Mhe. Maboto na Mhe. Getere kwa kututetea wananchi wa Nyatwali na kwa moyo huo tutawarudisha tena mjengoni mwaka 2025.