JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Upelelezi wa kesi ya uchochezi na kutoa taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii inayomkabili mwanaharakati na Mkurugenzi wa GH Foundation, Godlisten Malisa bado haujakamilika.
Malisa ameripoti leo Juni 18, 2024 katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro (RCO) baada ya kupewa dhamana Juni 8 mwaka huu katika kituo cha polisi kati mjini Moshi.
Malisa anakabiliwa na tuhuma tatu za kuchapisha taarifa za uchochezi kuhusu mauaji ya Beatrice Minja, mkazi wa Rombo anayedaiwa kuuliwa na mtu aliyekujulikana kwa jina la Paul Tarimo, tukio la mwanafunzi anayedaiwa kuuliwa kwa kichapo Moshi.
Nyingine ni tuhuma za kutoa taarifa bila kibali kwenye akaunti yake ya Instagram kuhusu walimu waliokuwa wakisahihisha mitihani ya kidato cha nne Januari, mwaka huu kuhusu kutolipwa posho zao.
Malisa alikamatwa Juni 6, 2024 muda mfupi baada ya kesi inayomkabili yeye na Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kuahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam na kusafirishwa hadi mkoani Kilimanjaro ambako alikuwa akikabiliwa na tuhuma hizo tatu.
Akizungumza na Mwananchi Digital leo Juni 18,2024 Malisa amesema baada ya kuripoti kituo cha polisi kati, Mjini Moshi ametakiwa kuripoti tena kituoni hapo Juni 27 mwaka huu, ili kujua hatma ya kesi hizo zinazomkabili.
"Leo tulifika ofisi ya Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro (RCO) kwa ajili ya kesi ambazo zinanikabili, ambazo ni kesi za mtandao kuhusu uchochezi na kutoa taarifa za uongo."
"Nimetekeleza wito huo na Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wametupa nafasi turudi tena siku ya alhamis Juni 27 ,2024 tunatarajia pengine upelelezi utakuwa umekamilika kwa wakati huo, hiyo tulienda kuripoti kama ilivyo ada kutii matakwa ya kisheria wa wito wa Jeshi la Polisi kwa sababu upelelezi haujakamilika, nimepewa nafasi yakuendelea na shughuli zangu na Juni 27, 2024 nitafika tena kwa ajili ya kujua hatma ya hii kesi ni nini ama vinginevyo," amesema Malisa.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma: Hatimaye Malisa na Boniface Jacob waachiwa kwa dhamana