BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Muda wangu wa kuchangia nimeutumia kujibu maswali matano yanayoulizwa na wengi huko mtaani kuhusu Katiba (5 common questions).
1. Kwanini mchakato huu umeandaliwa na BAVICHA? Mnapigania Katiba ya nchi au ya Chadema?
#Jibu: Mchakato wowote wa katiba ni wa kisheria na kisiasa. Katiba ni jambo linalogusa watu wote, hivyo kila kundi lina haki ya kujadili. Vijana wa chama cha zamani, badala ya kuwaonea gere BAVICHA, nanyi mnaweza kuandaa kongamano lenu. Muhimu kila mtu apate nafasi ya kuamua muastakabali wa taifa letu.
2. Katiba mpya sio kipaumbele cha Rais, kwanini msiachane nayo?
#Jibu: Katiba sio mali ya Rais ni mali ya wananchi. Hivyo kama wananchi wanataka katiba mpya, Rais hawezi kuzuia kwa namna yoyote. Kama wananchi wakisema Katiba mpya ni kipaumbele chao, Rais atake asitake atalazimishwa (kwa sauti ya kimbunga Jobo).
3. Je, Katiba mpya ina umuhimu wowote?
#Jibu: Ndio. Itatuwezesha kupata tume huru ya uchaguzi, ambayo mchezaji wa timu pinzani hataweza kujigeuza refa kama ilivyo sasa. Itaimarisha uchumi kwa sababu wawekezaji wote wakubwa duniani hupenda kuinvest mitaji yao mahali penye stability ya kisiasa. Pamoja na faida nyingine nyingi (ambazo zimetajwa na wazungunzaji wengine) katiba mpya itamfunga "breki" Rais asiteue majambazi kama Sabaya na kuwapa ofisi za umma.
4. Kwanini tusifanye marekebisho kidogo ya Katiba iliyopo badala ya kudai mpya?
#Jibu: Katiba iliyopo imeshafanyiwa marekebisho mengi sana. Kati ya mwaka 1980 hadi 1995 ikifanyiwa marekebisho mara 13. Kama ni nguo basi imechakaa na ina viraka vingi sana. Kwahiyo badala ya kutafuta mahali pengine pa kuweka kiraka, ni bora tununue nguo mpya.
5. Kwanini Mchakato wa Katiba usisubiri kwanza ili tujenge uchumi kama alivyosema mama Samia?
#Jibu: Wakati akiongea na waandishi wa habari, Mama Samia alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, uchumi wa nchi uliporomoka kutoka 7.2% hadi 4.8%. Kumbuka kipindi hicho mchakato wa katiba ulikua umesimamishwa. Kama kuzuia Katiba mpya kunasaidia kujenga uchumi, basi ilitakiwa kipindi cha mwendazake uchumi uimarike kuliko wakati mwingine wowote, lakini haikua hivyo.