Abul Aaliyah
JF-Expert Member
- Nov 8, 2016
- 7,718
- 5,899
Wanaodai katiba kwa nguvu sio wananchi ila ni CHADEMA idadi yao haifikii hata robo ya watanzania wote
Na hao CHADEMA wanadai hiyo katiba kwa tamaa yao ya madaraka wanahisi labda litakua daraja la wao kuingia madarakani na ndio maana wakuzungumzia katiba mpya wanalenga katika tume ya uchaguzi
In short ndio CHADEMA inakufa maana mtapoteza hi miaka 4 yote kudai katiba na hiyo katiba haitapatikana
R.I.P CHADEMA
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umewahi kuisikia katiba ya uk au kujua ilivo?? Jiulize ndo utatajua kuwa mifumo ipo tofauti Sana...Acha kujidanganya ww,mataifa mengi ya ulaya magharibi yalipata maendeleo makubwa baada ya mabadiliko ya kisiasa sambamba na katiba bora.
Hiv kwann chama chakavu mnaiogopa katiba mpya????yaan bdo mnataka hii mbeleko iliyopo ktk hii katiba chakavu?????
Mambo 2 makuu,Kwanza, mkuu wananchi kutokuelewa katiba yao ni uthibitisho tosha kwamba maendeleo ya kijamii katika nchi yetu ni mabaya sana mkuu. Kutokuelewa katiba yao maana yake hiyo jamii ina tongotongo kubwa sana katika macho yao.
Pili, kutokujua katiba yao inasemaje siyo hoja kubwa sana kwani huo ni uzembe wao. Sasa suala la uzembe wao wa kutokufuatilia mambo mbalimbali kwa manufaa yao yasikwamishe mchakato wa katiba mpya.
Tatu, mkuu katiba mpya tunayoitaka ni ambayo itaakisi maisha halisi ya Watanzania na yenye kuleta tija katika jamii na siyo ya copy & paste.
NB: suala la wananchi kutokujua katiba yao ya sasa ni uzembe mkubwa sana na siyo sababu ya msingi ya kutuzuia kuwa na katiba mpya.
Mkuu hoja ya katiba Mpya wewe unaiunga mkono?Kabla uongo wake wa list feki ya Lissu kulipwa mafao yake na bunge haujakauka vizuri leo malisa ameamua kuhara uongo mwingine!
Haya ngoja tuone mauzo ya cocaine yatqkavyokuwa mitaani baada ya punda kuachiwa huru na mahakama.
Mkuu umewahi kuisikia katiba ya uk au kujua ilivo?? Jiulize ndo utatajua kuwa mifumo ipo tofauti Sana...
Mkuu ninajidanganya vp???
Umejibiwa kwa manyik. Sema hautaki kusikia ukweli.Mkuu umejibu kwa hisia za kisiasa au kwa matink?? Kwa hyo Sasa hv tunaviongoz wabovu??
Ama kwa hakika CDM na BAVICHA ni "think tank" kwa maana ya kujali mustakabali mwema wa nchi hii. Kwa maana hiyo, CCM na UVCCM yake kumejaa "empty cases" wengi mno, hata mambo muhimu yaihusuyo nchi yao hawajali kabisa, zaidi ya chama chao kichakavu na matumbo yao wenyewe.Muda wangu wa kuchangia nimeutumia kujibu maswali matano yanayoulizwa na wengi huko mtaani kuhusu Katiba (5 common questions).
1. Kwanini mchakato huu umeandaliwa na BAVICHA? Mnapigania Katiba ya nchi au ya Chadema?
#Jibu: Mchakato wowote wa katiba ni wa kisheria na kisiasa. Katiba ni jambo linalogusa watu wote, hivyo kila kundi lina haki ya kujadili. Vijana wa chama cha zamani, badala ya kuwaonea gere BAVICHA, nanyi mnaweza kuandaa kongamano lenu. Muhimu kila mtu apate nafasi ya kuamua muastakabali wa taifa letu.
2. Katiba mpya sio kipaumbele cha Rais, kwanini msiachane nayo?
#Jibu: Katiba sio mali ya Rais ni mali ya wananchi. Hivyo kama wananchi wanataka katiba mpya, Rais hawezi kuzuia kwa namna yoyote. Kama wananchi wakisema Katiba mpya ni kipaumbele chao, Rais atake asitake atalazimishwa (kwa sauti ya kimbunga Jobo).
3. Je, Katiba mpya ina umuhimu wowote?
#Jibu: Ndio. Itatuwezesha kupata tume huru ya uchaguzi, ambayo mchezaji wa timu pinzani hataweza kujigeuza refa kama ilivyo sasa. Itaimarisha uchumi kwa sababu wawekezaji wote wakubwa duniani hupenda kuinvest mitaji yao mahali penye stability ya kisiasa. Pamoja na faida nyingine nyingi (ambazo zimetajwa na wazungunzaji wengine) katiba mpya itamfunga "breki" Rais asiteue majambazi kama Sabaya na kuwapa ofisi za umma.
4. Kwanini tusifanye marekebisho kidogo ya Katiba iliyopo badala ya kudai mpya?
#Jibu: Katiba iliyopo imeshafanyiwa marekebisho mengi sana. Kati ya mwaka 1980 hadi 1995 ikifanyiwa marekebisho mara 13. Kama ni nguo basi imechakaa na ina viraka vingi sana. Kwahiyo badala ya kutafuta mahali pengine pa kuweka kiraka, ni bora tununue nguo mpya.
5. Kwanini Mchakato wa Katiba usisubiri kwanza ili tujenge uchumi kama alivyosema mama Samia?
#Jibu: Wakati akiongea na waandishi wa habari, Mama Samia alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, uchumi wa nchi uliporomoka kutoka 7.2% hadi 4.8%. Kumbuka kipindi hicho mchakato wa katiba ulikua umesimamishwa. Kama kuzuia Katiba mpya kunasaidia kujenga uchumi, basi ilitakiwa kipindi cha mwendazake uchumi uimarike kuliko wakati mwingine wowote, lakini haikua hivyo.
- Katiba mpya ni takwa la kijamii, na linapata msukumo mkubwa na wanasiasa kwani katiba ni mchakato wa kisiasa.
- Katiba imeanza kudaiwa toka 1992 mfumo wa vyama vingi uliporejea hapa nchini. Huenda wakati huo hukuwa umezaliwa. 2010-2015 kulifanyika msukumo mkubwa wa kupata katiba mpya, hatimaye ilitungwa sheria ya mabadiliko ya katiba mpya, na tume ya Jaji Warioba ilizunguka nchi nzima, kukusanya maoni ya wananchi. Hatimaye kukawa na katiba pendekezwa ambayo ilikuwa inasubiri kupigiwa kura japo rasimu ya Warioba ilichezewa. Miaka mitano iliyopita nchi hii ilikuwa mikononi mwa rais muovu, aliyekuwa hataki katiba ya kumzuia kwenye uovu wake. Ila kwenye ilani ya ccm mchakato wa katiba pendekezwa ulikuwepo,lakini rais mwenye kiburi cha madaraka aliigomea. Tunashukuru Mungu kwa kutuondolea yule mtu muovu bila damu kumwagika.
- Katiba mpya italeta maendeleo maana itatoa viongozi wenye uhalali wa umma, na wataweza kuwajibishwa iwapo watakosea. nchi za Kenya, Afrika kusini na Ghana ni mifano halisi wa nchi zenye katiba bora, na zinaaminika hata na wawekezaji, kwani zinajali utawala wa sheria, na sio utashi wa rais aliye madarakani.
- Tume ya uchaguzi ni sehemu tu ya mapungufu ya hiyo katiba, lakini kuna madaraka makubwa ya urais ambayo yanatumika vibaya, na kwa maslahi binafsi ya rais na genge lake. Udhaifu huo umedhibitika wazi wakati wa JK, na rais muovu aliyefariki hivi karibuni.
- Bila utawala wa sheria ni ngumu muwekazaji makini kuwekeza, mfano hali ni wakati wa Magufuli wawekezaji wengi waliondoka. Kama hakuna wawekezaji ni ngumu uchumi kukua. Pia ni rahisi nchi kuingia machafuko ni, kwani hakuna haki. Kama katiba mpya haisaidii mtu wa kijijini, hayo maVX ya serikalini yanawasaidia nini hao wananchi?
Swali la ngapi majibu yake yana mianya doonUkiona umejibu swali, badala ya kufunga mianya ya maswali, inakuwa umefungua mianya ya maswali zaidi, maana yake jibu ulilojibu ni zuri lakini sio sahihi.
Majibu ya kaka yetu kipenzi Malisa ni mazuri ila yana mapengo kibao.
Namshauri apunguze hisia afanye tafiti aje na objective answers.
Kimsing nakuelewa walao Sasa Kama ndvyo umhim wa katiba mpya uanzie wapi?? Wakati katba ile ambayo mchakato wake ulikwama na hakuna sabba ya kwa nn ulikwama nlikuwa nafanya kazi maeneo tofaut ya kijijn.. baadhi ya watu nliokutana nao hawakuwa na uelewa walao hata wa neno katiba wengine waliniuliza hv hulo bunge la katiba maana yake Nini??
Kwa hyo kunakazi Kwanza ya kuielimisha jamii ya Sasa katiba maana yake Nini.. mapungufu yaliyopo kwenye katiba ya Sasa na kwa nn tutake katiba nyingine..
Na je tunaiunda Kama copy&pest ya ambayo haikufikia muafaka au tunaitaka tuunde ya kwetu??
Mkuu hatuundi katiba kwa kuangalia wengine wameundaje ya kwao ila jambo la Msingi tujue hasa mahitaji ya jamii yetu ni yapi..
Umesema vyema MAENDELEO si kuangalia tu binafsi ila ya ujumla.. na hapo ndpo tunapokuja na vipaumbele... Ni vyema tujiridhishe Kama kwel jamii ya Sasa kwa takwim halisi tunahitaji katiba??
Haa haa 😳😳😳😳haa,Ninayo maswal machache,
1) Hitajia la katiba mpya nilakisiasa, au la kijamii? Ukijibu njoo na majibu vivid
2) Kwanini katiba mpya uwe Sasa? Kwa Nini haikuwa miaka5 iliyopita? Nini kimepelekea kuidai sasa?
3) Eleza hoja yenye mashiko katiba mpya itasaidiaje kuleta maendeleo ya Tanzania na watanzania? Eleza japo kwa mifano hai ni nchi zipi kwa kuwa na katiba(nzuri) zinamaendeleo kwa sababu ya katiba?
4) Unakubali au kukanusha juu ya ukwel kuwa katiba iliyopo inapangufu katika tume ya uchaguzi na si katiba yote? Ukanushaji au ukubali uwe na majib yaliyo na vielelezo hai.
5) Tuambie kwa faida au kwa hasara Nini kitatokea kama tusipokuwa na katiba nyingine kwa miaka 10 ijayo? Mwananchi alieko kule nyakahoze au mugumu Serengeti au kule songwe kijijini ataathirika vipi?
Nasubri majibu
Mr bonny
Umekosea...Ndiyo maana tunapendekeza kwamba katiba itupe mamlaka sisi wananchi ya kuwaadibisha wanasiasa(Wabunge) ambao hawatendi wanachokiongea.
"Wanasiasa hawapendi SIASA ila wanapenda MADARAKA"Profesa Emeritus Isa ShivjiMkuu walao kiduchu umejib... Tatzo kubwa tu lipo kwenye maelezo na mifano.. hzo nchi zote ulizozitaja ukiwemo na Ghana... Maendeleo yal hayatokani na katiba.. ila inatokana na historia ya eneo...
Mfano...mapungufu yaliyopo yanaweza yasiwe takwa la kijamii ila la kisiasa.. ni mhim ukatambua kuwa jamii yote ya kinzania inaustarab wake.. kwa hyo haiwez ikawa ni sawa na wanasiasa...
Wanasiasa huwa wananuni ya kuongea one agenst 2... Wanachosema sicho wanachokitenda...
Mama anaupiga mwingi mnooMuda wangu wa kuchangia nimeutumia kujibu maswali matano yanayoulizwa na wengi huko mtaani kuhusu Katiba (5 common questions).