Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
Mkuu, hakuna hata moja ambalo limekugusa?Kasimama masaa mawili kuongea nonsense
Baba Antpass sema neno
huyu mama anauwezo mdogo sana wa kubambanua mambo .Nimesikiliza hotuba ya raisi akifungua rasmi bunge la 13 na nimeona ni kama ameanza kuinama na kujisitiri kutokana na yale yaliyotokea.
- Je, ili achutame kabisa kiungwana na kuepuka fedheha inabidi afanye nini?
- Kwa wenzangu mliosikiliza hotuba: je imewatia moyo au ndiyo imewaongeza hasira?
- Gen Z na wote wanaosapoti D9: kuna hoja hata moja imeongelewa ambayo inagusa malalamiko ya maandamano yaliyopita au yale yajayo?
Binafsi kwa niliyoyasikia nimeona ni inawezekana watawala wameona mabavu siyo suluhisho litakalotufikisha mahali pazuri kama taifa. Nafikiri haya mambo 5 yameashiria kwamba sauti za watanzania zina nguvu:
- Kukiri kuhusu mauaji ya siku za uchaguzi na kutoa pole
- Mchakato wa katiba mpya kurejea ndani ya siku 100 za kwanza
- Kufuta kesi za uhaini kwa vijana
- Tume ya kuchunguza mauaji ya Oktoba 29 na maridhiano (japo bado kna maswali:akina nani wapo hiyo tume na wamepatikanej)
- Kuanzisha wizara maalum ya vijana na ajira mpya sekta za elimu na afya
Mambo mengine niliyoyasikia ni blah blah za kila mwanasiasa - Mikopo, uboreshaji miundombinu , kilimo, utalii, uwezeshaji madini, kuinua uchumi, tehama, mwendokasi, reli, madaraja mapya etc.
Kilichonishangaza: ni wabunge kupiga makofi mengi pale raisi aliposema anywe maji kidogo 😂😂
Mama antpass Sina neno kwakweli Wacha nipite kama naaga maitiBaba Antpass sema neno
Wapi amefeli kwenye hii hotuba yake?huyu mama anauwezo mdogo sana wa kubambanua mambo .
Kaongea nonsense, moyo wangu una hasira kali dhidi yake.Mkuu, hakuna hata moja ambalo limekugusa?
alisha haribu tangu siku ile anaapishwa kusema waandamanaji ni raia wa kigeni then leo anatoa pole kwa wahanga daaaah inasikitisha sanaWapi amefeli kwenye hii hotuba yake?
Sawa, njia nyeupe baba 😅Mama antpass Sina neno kwakweli Wacha nipite kama naaga maiti
Labda anatoa pole kwa hao raia wa kigeni 🤷🏽♀️alisha haribu tangu siku ile anaapishwa kusema waandamanaji ni raia wa kigeni then leo anatoa pole kwa wahanga daaaah inasikitisha sana
Hawa jamaa waliniuliza taarifa za maandamano ulikuwa unazipata wapi nikawaambia jf.. ss kitendo Cha kulala na sim zangu wanaweza wakawa washadukua wanaijua I'd yangu. Hapo nadhani ni kuchange I'd tu niwe huruSawa, njia nyeupe baba 😅
Fanya hivyo usije kuingia matatani, hao wapuuzi siyo watu wazuri kabisa 🫤😬Hawa jamaa waliniuliza taarifa za maandamano ulikuwa unazipata wapi nikawaambia jf.. ss kitendo Cha kulala na sim zangu wanaweza wakawa washadukua wanaijua I'd yangu. Hapo nadhani ni kuchange I'd tu niwe huru