Malkia Cleopatra

Malkia Cleopatra

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
4,805
Reaction score
17,850
Cleopatra alikwea umalkia au kiti cha enzi akiwa na umri wa miaka 17 na alikufa akiwa na umri wa miaka 39. Alizungumza lugha 9. Alijua lugha ya Misri ya Kale na alijifunza kusoma maandishi ya kale ya kimisri(Egyptian hieroglyphs/sacred carvings), kisa cha pekee katika nasaba yake. Mbali na hayo, alijua Kigiriki na lugha za Waparthi, Waebrania, Wamedi, Troglodytes, Washami, Waethiopia, na Waarabu.

Kwa ujuzi huu, kitabu chochote duniani kilikuwa wazi kwake. Mbali na lugha, alisoma jiografia, historia, unajimu, diplomasia ya kimataifa, hisabati, alchemy, dawa, zoolojia, uchumi, na taaluma zingine. Alijaribu kupata maarifa yote ya wakati wake.

Cleopatra alitumia muda mwingi katika aina ya maabara ya kale. Aliandika baadhi ya kazi zinazohusiana na mitishamba na vipodozi. Kwa bahati mbaya, vitabu vyake vyote viliharibiwa kwa moto wa Maktaba kuu ya Alexandria mnamo 391 AD. Mwanafizikia maarufu Galen alisoma kazi yake na aliweza kunakili baadhi ya mapishi yaliyobuniwa na Cleopatra.

Mojawapo ya tiba hizi, ambazo Galen pia alipendekeza kwa wagonjwa wake, ilikuwa cream maalum ambayo inaweza kusaidia wanaume wenye vipara kurejesha nywele zao. Vitabu vya Cleopatra pia vilijumuisha vidokezo vya urembo, lakini hakuna hata kimoja kilichorithiwa na kizazi chetu.

Malkia wa Misri pia alipendezwa na uponyaji wa mitishamba, na shukrani kwa ujuzi wake wa lugha alipata papyri nyingi ambazo zimepotea leo. Ushawishi wake juu ya sayansi na dawa ulijulikana sana katika karne za mapema za Ukristo. Yeye, bila shaka, ni mtu wa kipekee katika historia ya ubinadamu.

IMG_20221102_224328.jpg
 
Andiko zuri.
Lakini uyo alikua ni Cleopatra yupi, maana Cleopatra ilikua ni kama title hivi.
 
Cleopatra alipiga vitabu hasa hivyo alikia mjanja sana alikua mzuri kweye diplomasia, Alianza kutumia kila mbinu kuikuomboa nchi yake Misri kutoka kwa Warumi.

Chakwanza alianza kujipendekeza kwa bedui Julio Caesars akamdanganya dangaya Dikteta kashikika wakawa wapenzi mzee baba Kaisari akawa anajilia Mtoto mzuri with Classy Cleopatra. Hadi siku Caesars anachomwa visu na maseneta wake Cleopatra alikuwepo ikulu Roma wengine wanasema nae alishiriki kwenye njama za kumuua Julio Caesar ila uhusiano wao ulileta mtoto wa kiume aitwae Caesarion ambae nae alikuja kuwa mtawala wa Roma (?).

Bado mwanadada aliendelea kutumia uzuri wake kuwapagawisha viongozi wa rumi ili kutafuta jinsi ya kuikomboa nchi yake.

Cleopatra kazama mapenzini na Marcus Antonius (Mark Anthony) yaani walipendana hadi Mark akamuacha mkewe Octavia amabe alikua dada wa Octavian/Agusto.

Mark Anthony akaagizwa aende misri kudai ile kodi ambayo watawala wamisri wanatakiwa wailipe Mark alipofika huko akazama penzini kwa Clepatra. wanakwambia Cleopatra alitumia mwaka mzima kula bata la nguvu (Luxury) na mpenzi wake Mark Anthony huku wakiwaacha wamisri/wananchi kwenye ufukara wa kiwango cha kabisa. Hawakuiahia hapo tu Mapenzi yaliwatuma kwamba ili wawe huru na penzi lao inabidi waivamie Roma waipige na kuichukua waendeleze kula bata la penzi lao.

Kule Roma taarifa zikamfikia Kaisari Agusto yaani aliyetumwa pesa kapewa penzi kanogewa kasahau kurudi lakini hajaishia hapo anapanga mbinu za kuvamia wenzake-Nchi yake kwa shinikizo la mapenzi/penzi la Cleopatra. Kaisari akaona dharau akatuma majeshi yakaenda misri yakagawa kichapo cha nguvu...Yaani Cleopatra na Mark walichapwa hadi wakakimbia wakajifungia ndani wakanywa sumu na kujiua. Octavian/Augusto alifika mwenyewe Alexandria na kuitawala hakuishia hapo kwa hasira alichoma ile Library/maktaba ya kwanza kujengwa duniani akaunguza kila kitu.. Ila hakua mjinga jamaa alibeba maarifa makubwa/Vitabu akahamishia Roma.
 
Tisha sana mkuu[emoji109][emoji109][emoji109]
 
Mbona wanasema aligongwa na Nyoka
 
Inasemekana alikuwa pisi kali kweli kweli.
 
Sio kweli mkuu, ni vile tu watu walikua wanapenda classy/Status yake as a Pharao of Egypt. Ajili ya cheo cha ssh kuna watu wanamuona ni pisi kali eti🏃🏃
 
Back
Top Bottom