Malkia wa Sheba(Queen of Sheba)

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
1Wafalme 10.7
Lakini mimi sikuzisadiki habari hizo hata nilipokuja na kuona kwa macho yangu; Tena tazama sikuambiwa nusu wewe umezidi kwa hekima na kufanikiwa kuliko habari nilizosikia.

Malikia wa Sheba anakubali na kuridhika juu ya hekima na busara za Mfalme Suleimani na hiyo ni baada ya kujibiwa maswali yake yote magumu katika kiwango ambacho hakukitarajia.

Je, Malkia wa Sheba ni nani?

Biblia imemtambulisha malikia wa Sheba kama kiongozi Mwanamke mtawala wa falme za Sheba aliyefunga safari kutokea ardhi ya Sheba akiambatana na watumishi, ngamia na kubwa zaidi ni Vito vyenye thamani kubwa kuelekea yerusalemu na lengo kuu la kumpa changamoto(challenge) Mfalme Suleimani ambaye habari za hekima na busara zake zilikuwa zimezagaa wakati huo.

Kuona ni kuamini hatimaye malikia wa Sheba anayashuhudia Yale aliyokuwa akiyasikia juu ya hekima za Mfalme Suleimani tena to the maximum. Ili kuonyesha appreciation zake malikia anampa Mfalme Suleimani Vito vya thamani ambavyo havijawahi kushuhudiwa hapo kabla katika ardhi ya yerusalemu. Katika Hali ya kurudisha fadhila Mfalme Suleimani anampa zawadi malikia wa Sheba na akikisho la kumpa chochote kile atakachohitaji.

Je, wapi ni ardhi ya Sheba uarabuni(Yemen) ama ni Africa(Ethiopia)?

Bado Kuna mvutano juu ya wapi ulipokuwa ufalme wa Sheba wataalamu wa mambo ya kale wanataja Yemen ya sasa kuwa ndipo ulipokuwa ufalme wa Sheba madai hayo yanapingwa vikali na Ethiopian Orthodox.

The Kebra Nagast(The glory of kings) ni maandiko muhimu ya kanisa la Ethiopian Orthodox, inamtaja malikia wa Sheba kama malikia mrembo anayefahamika kama Makeda na kutambua ardhi ya Sheba kuwa ni Ethiopia ya Sasa.

Kutokana na Kebra Nagast Malikia Makeda alisafiri kuelekea yerusalemu na alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mfalme Suleimani. Baadae Makeda anarejea katika Ardhi ya Sheba akiwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kiume aitwaye Menelik.

Menelik alipotimiza umri wa miaka 22 anasafiri kuelekea yerusalemu kukutana na baba yake. Mfalme Suleimani anafurahi kumuona mwanae na anamshawishi kubaki yerusalemu amrithishe ufalme Bali Menelik anachagua kurejea katika ardhi ya Sheba. Mfalme Suleimani anawaagiza watu kumsindikiza mwanaye mpaka Sheba na kumkabidhi Sheria(the art of the covenant).

Ethiopian wanaamini na kudai malikia wa Sheba ni sehemu ya urithi wao. pia wanaamini neno Sheba limetokana na neno Shaba(Cooper) kutokana na eneo hilo kuwa na utajiri wa madini hayo.

Mpaka Sasa inaendelea kuwa nadharia hakuna hitimisho wala uthibitisho juu ya nani ni Malikia wa Sheba? Na wapi ulipokuwa ufalme wa Sheba?

From northern part of Tanzania.
 
Mi nahisi hii miji inayotajwa kwenye vitabu vya dini, sio miji tunayoifikiria sisi. Wala hizo falme zinazotajwa hazikuwa kubwa, inawezekana ni kama walivyokuwa machifu wa huku kwetu. kwamba kila chifu ni mfalme!
 
Sipingani isipokuwa Si kila kiandikwacho ni kweli. Jee ni nani aliandika habari hiyo?
Ikiwa unajua kuwa si kila kiandikwacho ni kweli basi hukupaswa kuleta hapa hii story ya queen of Sheba maana sio kweli (kwa mtazamo wako)

Ila Biblia ni neno la kweli, ikiwa huamini kuwa ni neno la kweli basi acha kusambaza story zake kama hiyo ya queen.
 
Sikuleta mimi hii Story,Sorry hujajibu Nani kaandikar hiyo story ?
 
Unaposema biblia ni neno la kweli umekusudia biblia ipi ? Biblia ya Mormon, Ya Jehovas witness? Ya Queen James Version , ya King James Version , ya wa Katoliki Douay, au ipi katika maelfu ya biblia tofauti ?
 
Bethsheba ni mke wa Daud (mama mzazi wa mfalme solomon)..
Huyu ni malkia Makeda(bilqis)wa sheba binti wa malkia ismeni wa Ethiopia...
Bethsheba alikuwa ni mke wa Uria, alivyokufa Uria kwa hila za Mfalme Daudi kule vitani ndipo Daudi anamchukua na kuzaa naye watoto, among them ni Mfalme Solomon. Daudi alimuudhi Mungu kwa kutenda dhambi hii.
Ni maelezo tu ......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…