Malori manne ya mafuta yakamatwa yakiingiza vipodozi vilivyopigwa marufuku Nchini, mzigo umetokea DRC

Malori manne ya mafuta yakamatwa yakiingiza vipodozi vilivyopigwa marufuku Nchini, mzigo umetokea DRC

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Malori manne ya mafuta ya Kampuni ya Lake Oil yamekamatwa Mkoani Songwe yakiwa yamebeba shehena ya vipodozi vilivyopigwa marufuku Nchini ambayo yalikuwa yakitokea DRC huku madereva wa magari hayo wakiyatelekeza.

Meneja Ukaguzi wa Kampuni ya Lake Oil, Ali Sharif amesema magari yao yana mfumo wa GPS ambapo kuna mfumo wa kuziona popote zilipo, waliona zimeingia sehemu wasizozifahamu wakaanza kuzifuatilia, zilipofika Songwe wakazifanyia ukaguzi na kubaini hali hiyo.

“Magari mawili tumeyakamata tunayo hapa na mawili tumeshayazuia yapo Mbeya,” anasema Sharif.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omari Mgumba aliyekuwepo katika kituo hicho anasema: “Chemba zote za mafuta zimejaa vipodozi, tutaendelea kushikilia mzigo na madereva watuhumiwa, gari tutaziachia kwa kuwa wahusika wameonesha hawafurahishwi na kitu hiki na wametoa ushirikiano.”

Baadhi ya madereva wa magari makubwa ya mizigo wamedai kuwa wenzao wamefanya hivyo kutokana na malipo madogo wanayoyapata kutoka kwa waajiri wao.

Chanzo: ITV
 
Kula kwa urefu wa kamba ingawa risk
 
Tunahitaji mfumo mpya kwenye hizi border post zetu,ni muhimu tukawa na scanners na tunahitaji chombo kimoja kiwe kinasimamia hizi borders sio kama sasa kila dept inafanya kazi kivyake, angalia border control za Australia au New Zealand zote zipo chini ya umbrella moja,na unaanza kwanza na custom na hawa wakisha kuruhusu ndio inaenda immigrations not other way round, tayari una entry stamp on your passport then unaenda custom!
 
Mbinu ya kitambo na watu washatajirika hadi wakakosa pesa
 
Back
Top Bottom