Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Akizungumza kwa kujiamini mmoja wa wachangiaji amepinga kuvunjwa kwa jiji kulikoleta mkanganyiko wa hadhi ya maeneo , kwa kutolea mfano wa Chanika kuwa jijini huku Magomeni , Kinondoni , Masaki , Temeke , Mwenge na Mbezi Beach kuwa nje ya jiji .
Ametoa plan ambayo kama ingefanyiwa kazi basi mkanganyiko huo usingekuwepo na bado matumizi yangeendelea kubanwa , amedai kwamba kama lengo lilikuwa ni kubana matumizi ilikuwa rahisi tu kubadili muundo wa Jiji ambapo amependekeza vikao vya jiji vingekuwa vya mameya wa manispaa zake kwa lengo la kujadili palikofikiwa kwenye mipango ya manispaa hizo , bado jiji lingeendelea kuwepo bila kuipromote Buguruni kwa Mnyamani na kuitupa Oysterbay .
Mwisho mchangiaji huyo amekiri kufahamu mamlaka ya Rais na amesema hapingi mipango yake