Malumbano la hoja: Mchangiaji ashangaa jiji la Dar kuvunjwa kwa kisingizio cha kubana matumizi , ashangaa Chanika kuwa jiji magomeni kuwa nje ya jiji

Angalia hata taarifa za serikali
1. Jiji la ilala
2. Manispaa ya kinondoni
3. Manispaa ya temeke
4. Manispaa ya ubungo
5. Manispaa ya kigamboni
Kwahiyo jiji ni ilala tu.
Wewe umeelewaje labda?
 
Bado kidogo mtasikia wilaya mipya ya katoro.
 
Ukisema jiji la ilala tayari umeshaitoa Oysterbay, Masaki, mikocheni, mbezi beach, kijitonyama e.t.c
 
Kuondoa halmashauri ya jiji kwa sababu ina-overlap halmashauri za manispaa ni jambo la maana. Overlap hiyo ilitengeneza redundancy, hivyo cost ilikuwa kubwa wakati hakuna ulazima wa halmashauri hiyo iliyokuwa kama blanket.

Tatizo ni vile walivyoamua kipande kile pekee cha halmashauri ya ilala ndo kiwe chini ya halmashauri ya jiji. Wangefanya extension ya eneo la halmashauri ya Ilala, au ikiwezekana kugawa Dar Es Salaam upya ili ku-condolidate maeneo yote ya hadhi ya jiji itengenezeke yawe chini ya halmashauri ya jiji, na maeneo yaliyobaki yafanywe halmashauri ya hadhi za kimanispaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…