Mama alieuza watoto miaka ya 1948

Military Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2019
Posts
761
Reaction score
1,464


Kwa mara ya kwanza picha hii ilionekana Indiana US augost 5, 1948 ikionyesha kuna watoto wanne wamekaa mbele ya bango lenye maandishi '4 children for sale' yaani 'watoto wanne wanauzwa' na pembeni yake akiwa amesimama mama yao aliyeziba sura yake.

Chini ya maneno hayo kuliandikwa maneno mengine madogo 'inquire within' yakimaanisha kuwa unaweza kuuliza ili upate maelezo zaidi.

Mama yao aliyekuwa anaitwa Lucille Charifoux raia wa Chicago alieleza kuwa baada ya mumewe Ray kufukuzwa kazi ya udereva mgodini walifukuzwa pia katika nyumba waliyokuwa wamepanga, hawakua na sehemu ya kuishi, pesa wala chakula, na walikuwa na watoto wanne.

Maamuzi waliyoyafikia kwa pamoja yalikuwa ni kuwauza watoto wote, ni kweli wakaridhia kuwapiga bei watoto wao wanne ambao ni Lana (6), Rare (5), Milton (4) na Sue Ellen (2).

Cha kustaajabisha ni kuwa mama yao aliyeonekana pichani akiwa ameziba uso wake wakati huo alikuwa ni mjamzito, walipanga kuwa hata mtoto huyo atakaezaliwa watampiga mnada pia. Kabla hata hajazaliwa walimpa jina la David.

Baada ya kuliona tangazo hilo ndugu wa mwanamke huyu walimshitaki Luc kwa kutangaza kuwa anawauza watoto, na alikuwa ameshawauza kweli, haikujulikana ni nini kilitokea, maana miezi michache tu baada ya kujifungua na mtoto kubebwa mumewe Ray akafariki kwa mshtuko kwa kuwauza watoto wake.

Miaka ya 1940 maisha Amerika yalikuwa magumu mno kutokana na vita ya pili ya dunia kuleta uharibifu na ukosefu wa chakula, hata baada ya vita kuisha mwaka 1945 bado maisha yaliendelea kuwa magumu maradufu.

Mamilioni ya raia nchini humo walifukuzwa kazi na kuharibiwa nyumba zao, familia ya Charifoux ikiwemo.

Haijulikani wengine walinunuliwa kwa pesa ngapi, lakini Rare na Milton waliuzwa kwa mfanyabiashara Zoeteman wa mjini humo ambaye alisema anawanunua tu aende kuishi nao kutokana na ugumu wa maisha ambao wangeendelea kupitia iwapo wangebaki kwa mama yao.

"Mama aliniuza kwa $2, ilikuwa ni pesa ndogo sana" alingumza Rare mwaka 2013, dollar 2 ni sawa na shilingi 4,500 hivi ya Tanzania.

Rare ambaye alikuwa ni mtoto wa kike alisema kuwa hali ilienda kuwa tofauti kabisa katika maisha yao mapya nyumbani kwa Zoeteman, kwani walianza kulazimishwa kufanya kazi ngumu mashambani kwa masaa mengi wakiwa bado wadogo.

Akiwa na umri wa miaka 17 Rare alitekwa na kubakwa kitendo kilichopeleka apate ujauzito, hapo ndipo Zoeteman akamfukuza na kusababisha ugumu wa maisha kwa binti huyo kuongezeka maradufu. Baadaye akaenda kuishi katika kituo maalumu cha kuwalea mabinti wenye ujauzito.

Kaka yake Milton aliendelea kuishi kwa mateso makali katika familia ya mfanyabiashara huyo hali iliyopelekea kuathirika kisaikolojia hata wakati akiwa mkubwa, anasema alitumia muda mwingi sana kuishi katika hospitali za utimamu wa akili.

Rare pamoja na kaka yake Milton hawakuwahi kuonana tena tangu Rare afukuzwe na ujauzito akiwa na umri wa miaka 17 tuu, walikuja kuonana kwa mara nyingine tena mwaka 2013 wakiwa wazee tayari, dada yao Lana yeye alifariki kwa kansa mwaka 1998.

Mwenzao mwingine Sue Ellen alinunuliwa na familia ya Johnson ambapo baadaye mwaka 2013 naye alifanikiwa kukutana na wenzake hao wawili, bado alikuwa nayo gauni yake aliyovaa utotoni siku wakati anauzwa.

Mdogo wao David waliyemuacha bado hajazaliwa aliuzwa kwa familia ya Harry McDaniel ambao hawa walikuwa ni watu wazuri tuu waliopenda kuwasaidia watoto waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu.

Baada ya kuwauza watoto wake wote watano mama yao aliolewa mbele na kupata watoto wengine wanne wakike. David alisema kuwa baada ya mama yao kuwauza hajawahi kuwasiliana nao, aliwajali watoto wake wapya pekee huko alikoolewa.

Milton na dada yake Sue Ellen walisema katu hawatokuja kumsamehe mama yao huyo. Milton alisema mama yao aliwachukia sana, aliwauza na katu hakuwahi kuwatafuta hata kuwasalimia au kuwaomba msamaha, kwahivyo wao hawatamsamehe kamwe.

Ellen yeye alisema mama yao huyo itapendeza kama atachomwa na moto milele jehanamu baada ya kufariki, huku mdogo wao David akiwa ameharika akili kwa msongo wa mawazo ya muda mrefu juu ya tukio hilo walilowahi kufanyiwa na mama yao, anasema hajawahi kuacha kuwaza.

"Hakuwahi kututafuta na kutuomba msamaha, sisi wote ni binadamu, maana yake alipenda sisi tufe, hakujali kuhusu sisi", Wote wanne walikutana mwaka 2013 kwa Mara ya kwanza tangu wauzwe, dada yao mkubwa Lana alifariki mwaka 1998 akiwa na umri wa miaka 56.

Written by Military Genius
 
Inachekesha ila ni story ya kufundisha sana.
nina jembe langu nilikuwa nafikiria kuliuza sumbufu sana limeanza kufunua watoto wenzie
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] unasubir nn ss

πŸ…œπŸ…˜πŸ…›πŸ…˜πŸ…£πŸ…πŸ…‘πŸ…¨ πŸ…–πŸ…”πŸ…πŸ…˜πŸ…€πŸ…’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…