Fatuma Iddi (mama wa watoto wanne) mkazi wa Magugu Mapea, Babati amerejeshewa tabasamu na Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi CCM Ally Hapi baada ya kupewa mtaji wa kufanya biashara.
Fatuma alivunjiwa kibanda (duka dogo) na banda la kuonyesha mpiria alilokuwa akimiliki na mumewe kwa madai ya kuwa kibanda hicho kimenunuliwa na mtu mwingine.
Fatuma amedai kuwa alipewa taarifa kuwa mumewe alishiriki kuuza kibanda hicho na alikimbia mpaka pale aliposikia kuwa anatafutwa ndipo akarudi.
Ally Hapi amempa mama huyo mtaji wa takribani 250,000/= huku akimtaka kuanza kufanya biashara ndogo ndogo na kumsamehe mumewe ili kuepusha ugomvi zaidi.