Chapa Nalo Jr
JF-Expert Member
- Dec 8, 2010
- 7,518
- 6,506
Daa afu nilishakujibu kule kumbe umekuja huku kabisa bwana, haya lakini ukweli ni ule ule, hakuna siri kwenye ndoa na mshauri wako wa kwanza ni mume wako.Kwa sababu yeye ndo ubavu wako, haiwezekani mume wako akaombe pesa ya matumizi kwa mkwe wake, au asijue miradi ya mke wake. Yani vaisi vesa ni true.
Kama yanatoka moyoni na wake wote ndio msimamo wao basi ni vema sana; nimeuliza hivi kwa sababu kuna malalamiko ya wanaume (hata hapa JF) kuwa wanawake kuiona hela yao au kuchangia hela yao ni mbinde
Pili nilishakuwa na mjadala na dada mmoja mwanasheria na ameolewa. Hoja ilikuwa sheria ya ndoa TZ inasema ndoa ikivunjika basi mme ataendelea kutoa matunzo kwa mke mpaka atakapoolewa tena au vinginevyo(sic), lakini sheria haisemi chochote kama ndoa husika mwanamke ndio mwenye hela. Sasa huyo dada alipinga kabisa sheria hiyo kurekebishwa ili na mwanaume apewe matunzo na ex-wife, yaani hakutaka hata kutoa sababu. Je Ulimwengu kweli upo tayari kwa usawa unaopigiwa kampeini!!!?
Kama kuna USAWA kati ya mwanamke na mwanaume hiyo sheria irekebishwe!Na kama wanaume mtakua na amani kulishwa na mwanamke ambae hata mahusiano hamna!!Nwyz kuhusu mali mkiwa pamoja kuwa na siri sio sahihi!Iwe mwanamke au mwanaume ndo mwenye hela mwenzake ana haki ya kufahamu na hata kusaidia kama kuna miradi!Kuna mahali nilisema..kama MAWAZO YA MIMI..CHANGU VYANGU bado yamekutawala usioe wala kuolewa!Subiri mpaka utakapokua tayari kushea kila kilicho chako na mwenzako!
Binafsi naamini, hakuna usawa utakao tokea duniani kati ya mwanamke na mwanaume. Mwanaume atabaki kama mwanaume na atamtawala mwanamke na tamaa yake itakuwa juu ya mwanamke!! (Biblia kitabu cha mwanzo). Lakini hamtuonea bila sababu kwa sababu tunapakusema na tunaweza kuongea sasa. Kwa hiyo mwanaume inabidi apigane na maisha kweli kweli. Kwa sababu kwa jinsi mlivyoumbwa mwanamke akiwa juu yako kidogo tu, hamwezi kuwa na amani wala uhuru nafsini mwenu.
Kama maandiko yangefuatwa kwa usahihi mbona mambo yangeenda sawa mno, lakini kuna watu wanachagua vifungu fulani tu vya maandiko na vingine hawataki hata kuvisema. Kuna members humu JF aliwahi puuza hata uwepo wa Mungu na akasema ni Mungu gani huyo eti anayezidiwa hekima ya usawa na binadamu!!. Naamini ndoa zinazofuata maandiko matakatifu kwa usahihi huwa hazikumbwi na dhoruba na kuvunjika.
Hapo kwenye redi, mbona wanawake wanalishwa kwa mujibu wa sheria na ma ex-husband wao, je wao wana amani? Kwa sababu katika hati za talaka wanawake huwa hawasahau ilo ombi la matunzo kupitia mahakama. Acha tu sheria irekebishwe ili mwanaume ataeamua kutodai sawa, ataedai sheria imlinde.
Kama tu kuoa mwanamke mwenye pesa zaidi ya mwanaume wengi wenu mnaona tabu kulelewa ndo itakua afadhali!!???:twitch: