Mama Diamond, Wolper wafunika kwenye video mpya ya Diamond

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Kuna msemo usemao experience is the best teacher, msemo huu umekamilika kupitia mama mzazi wa msanii diamond platnums , baada ya kuigiza kama mama ambaye ana maisha magumu kupitiliza,huku akiwa ameuvaa uhusika vilivyo kupitia video mpya ya msanii huyo ambaye ni mwanae wa kumzaa huitwao, je utanipenda.

Mama diamond, ni kati ya watu wachache waliotumika kwenye video hiyo na kuifanya ionekane kuwa na mvuto wa kipekee na kubeba hisia za mamilioni ya watanzania kwa uchezaji wa hali ya juu alioonyesha kwenye video hiyo.

Mbali na mama diamond, msanii wolper nae anatajwa kuhusika kwa namna moja au nyingine kuifanya video hiyo kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na uchezaji wake wa nyodo na dharau,hulka iliyomvaa vilivyo na kuitendea haki.


Mashabiki wengi waliyoiona video hiyo wamempongeza sana mama diamond kwa kuvaa uhusika, na kumtabiria kufanya vyema kwenye sekta ya uigizaji kama akiamua kuingia huko.
 

Attachments

  • 1449986440396.jpg
    85.1 KB · Views: 1,902
Video nimeielewa vya kutosha but audio kwangu ziiii, sijui vile nimezoea za kuchezeka!!??
 
Ndioooo.. Zari nae ametisha sana, Babu tale hahahaha, harmonize katishaaa....

Bi sandra kawavuta wengi kwasababu ya scene yake ilivyo ya kusikitisha zaidi hasa ukizingatia alikuwa kabeba mtoto na ile facial expression daaah lazima uhuzunike..

Mi nimependa sana maeneo ya dakk 3:02 hiviii pale diamond yupo na zari wanaingia wanawapa watu salamu hiviii wametisha sana pia, pamoja na kakipande ka mwisho ka kujidai Tudy na vinanda jins Chibu anatoka na mtoto mzuri na anavyocheza pale...

Ni nomaaaa, UTANIPENDA..!!
 
Video nimeielewa vya kutosha but audio kwangu ziiii, sijui vile nimezoea za kuchezeka!!??

Sasa kama unataka nyimbo za kuchezeka huwezi kusema umeuelewa huu... Huku ndiko alikotokea Diamond, na ndio tuliko mpendea saaaana kabla hajaanza na za kuchangamka kama Moyo wangu...! Mashabiki tunahitaji tucheze, na tupate kitu cha taratiiibu cha kuimba at the sama time maana sio kila muda unakuwa na mood moja

Na huu wimbo umemuongezea sana mashabiki hasa wa kike, suala la kuimba na kuwafanya hadi wansume walie sio dogo kabisaa..
 

Yani una mahab first Class.
Du
 
da Wolper anajodo,babu tale wacha akimbie,nilicheka kisenge.pa harmonize pale uzuni tu mshikaji kakata cmu .
 
Shikamooo da ngote ukweli uw a ukosei umelenga maisha yanavyo kuwa after kufulia na hili limekuwa sugu sana marafiki wa Leo ukiwa nazo ndo mahadui wako Wa kesho
 
Kwa ujumla nyimbo imekamilika sehemu zote kwenye audio yake hadi video na mashairi yameenda shule meseji ya kuuzunisha biti tamu sana na walioshiriki kwenye video wameuvaa uhusika mno na huyu mama yetu ndio kamaliza kazi kabisa bila kumsahau,wolper,harmonize,tale,mwana fa,mlinzi,mkubwa fellah, na wengine wengi wameufanikisha MZIGO KUWA WA MAANA ZAIDI HONGERA SANA DIAMOND KWA KUTULETEA BONGE MOJA LA NGOMA.
 

Nadhan kwa kuwa Yale maisha kashayapitia ndio maana haikua kazi kwa Kama diamond Ku express feelings zake, yani dah katishaa
 

mkuu taste zetu zinafanana kabisa kwenye huu wimbo yani pale mwisho mwisho...vile vinanda na the way jamaa anacheza pamenifurahisha saaanaa,dogo cjui huwa anafikiriagaje aise mpk anapekenyua mavitu adimu kama haya...!
 
mbona mimi sijapata huo wimbo. nikiujaribu youtube unazingua
 
mbona mimi sijapata huo wimbo. nikiujaribu youtube unazingua

Kama youtube haupati ingia katika website ya tooxclusive.com au notjustok.com za nigeria utaupakua mzigo tena ukiwa na english subtitles
 

Mhh kipendacho roho......kumbe ndo hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…